ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 21, 2018

TAASISI YA MAENDELEO JIMBO LA VUNJO (VDF) YASEMA GHARAMA UKARABATI WA BARABARA NDANI YA JIMBO HILO HUENDA ZIKAONGEZEKA ZAIDI

Katibu wa Taasisi ya Maeneleo ya Jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa salamu kwa baadhi ya wananchi walioshiriki katika ukarabati wa miundo mbinu ya barabara unaoendelea katika jimbo hilo kwa kuchangia nguvu kazi.
Mmoja wa wananchi waliojitokeza katika ukataji wa miti kupisha upanuzi wa barabara akiandaa mbao kwa ajili ya shughuli nyingine za uakarabati wa barabara hizo. 

Greda likiendelea na kazi ya uondoshaji wa baadhi ya miti iliyokuwa kando ya barabara zinazopanuliwa katika jimbo la Vunjo.
Mafundi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiondosha Nyaya ili kupisha upanuzi wa barabara hizo.
Shughuli ya upanuzi wa barabara ikiendelea.
Baadhi ya wananchi wakichangia nguvu kazi katika ukarabati wa barabara hizo.
Upanuzi wa barabara mbalimbali ukiendelea katika jimbo la Vunjo. 
Moja ya eneo ambalo kazi ya upasuaji wamiamba ililazimika kufanyika ili kupanua barabara .
Muonekano wa barabara katika maeneo mbalimbali wakati ukaraba huo ukiendelea .


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

TAASISI ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo(VDF) imesema gharama zilizotengwa awali kwa ajili ya ukarabati wa Km 272.8 za barabara katika vijiji vyote vya jimbo hilo huenda zikaongezeka kutokana na kuwepo kwa miamba katika maeneo ambayo yanahitaji upanuzi.

Katibu wa taasisi hiyo,James Mbatia amesema ikiwa imengia wiki ya tatu tangu kuanza kwa ukarabati kwa baadhi ya maeneo katika barabara hizo tayari wamekutana na changamoto ya uwepo wa miamba ambayo imelazimika kuvunjwa kwanza .

“Tulipanga hii kazi kutumia miezi sita kuimaliza lakini sasa inaweza kuchukua hadi mwaka mmoja kutokana na changamoto ambazo zimeanza kujitokeza hizi za kukutana na miamba na wakati mwingine hali ya hewa”alisema Mbatia.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo alisema awali walipanga kutumia kiasi cha Sh Bil 7.29 kukamilisha kazi hizo lakini kwa namna shughuli inavyoendelea huenda gharama ikazidi huku akiendelea kutoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia

“Hadi sasa tunashukuru kazi inaendelea vizuri tukishirikiana nawenzetu wa TARURA,TANESCO na tasisi nyingine ,lakini kipekee niombe serikali ione umuhimu wa kusaidia katika kutatua changamoto hii ya barabara kwa wakazi hawa wa jimbo la Vunjo”alisema Mbatia.

Kutokana na kuendelea kwa shughuli ya ukarabati wa barabara hizo tayari wananchi katika vijiji vya Shira na Mshiri vilivyopo katika jimbo la Vunjo wameanza kunufaika na mradi huo unaotekelezwa na Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo (VDF).

Shughuli ya upanuzi wa barabara katika kijiji cha Mshiri,Marangu ikiendelea kwa uondoaji wa miti iliyo kando ya barabara ya awali sambamba na uondohaji wa Miundo mbinu ya umeme ili kupisha shughuli za upanuzi.

Michuzi Blog  imefika katika maeneo mbalimbali ya vijiji vilivyoko katika jimbo la Vunjo na kujionea mitambo ikiendelea na shughuli za upanuzi wa barabara pamoja na uondoaji wa miti na mawe makubwa yaliyokuwa katika maeneo ya barabara hizo.

Happy Makyao na Neema Temu ni wakazi wa Marangu ambao wanajishughulisha na biashara ya matunda katika eneo la Marangu Mtoni wakazungumzia adha walizokumbana nazo kabla ya kuanza kwa ukarabati huo na matumaini yao mara baada ya kukamilika kwa mrad huo.

“Kabla ya matengenezo ya hizi barabara tulikuwa tikipata shida sana kutokana na baadhi ya maeneo kuwa na vichaka vikubwa na wakati mwingie ilikuwa ni hatari kwa wanafunzi na wakati mwingine walibakwa kwa sasa tumeanza kuona unafuu mkubwa”alisema Happy Makyao.

Kwa upande wake Neema Tema aliipongeza taasisi ya VDF kwa kazi kubwa waliyoianza katika jimbo la Vunjo na kwamba kwa sasa maeneo ambay yalikuwa hayafikiki kwa urahisi na kwa gharama ya juu sasa yanafikika.

“Kwa mfano bidhaa zetu tukizisafirisha kutoka maeneo ya juu kuja hapa Marangu Mtoni ,tulikuwa tunatumia kiasi cha Sh 2000 hadi 3000 kwa kutumia pikipiki lakini kwa sasa baada ya kufanyika ukarabati tunalipa sh 1000.”alisema Temu.

Exaud Mamuya Diwani wa kata ya Mshiri,Marangu akaeleza juu ya fursa kwa wananch hao zinaoztokana na ukarabati wa miundo mbinu ya barabara katika maeneo yao kwa kukusanya mawe yaliyochimbuliwa na kisha kuyauza.

“Matengenezo haya ya barabara yametoa Fursa pia kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara hizo,mfano kupata kibali cha kukata mti wako ilikuwa lazima uingie gharama ,lakini kwa sasa wananchi wanaweza kukata miti yao kwenye maeneo ambayo barabara zinapanuliwa”alisema Mamuya.

“Eneo jingine ambalo wananchi wananufaika nalo ni wakati wa upanuzi wabarabara kuna Mawe ambayo yamekuwa yakiondolewa barabarni ,wananchi wamekuwa wakiyakusanya na kuyauza ambapo wamekuwa wakipata hadi sh 80000 kwa lori moja”aliongeza Mamuya.

Kuanzishwa kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo (VDF) kutasaidia utatuzi wa kero katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji ambapo kwa upande wa miundo mbinu ya barabara,Km 272.8 za vijiji vyote katika jimbo hilo zinataraji kupitiwa.

Mwisho.

No comments: