ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 30, 2018

WILAYA YA MPWAPWA KUTUMIA ZAO LA KOROSHO KUJENGA UCHUMI

 MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Jabiri Shekimweri kushoto akizungumzia na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana mikakati yao katika zao la Korosho wakati wa ziara ya viongozi wa bodi hiyo kutembelea maeneo mapya kuhamasisha kilimo hicho
 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akisisitiza jamabo kwa Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kuhusu ziara yao wilayani humo
  Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akiagana na Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodomaa mara baada ya kumaliza mazungumzo

 Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri katika akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa bodi ya Korosho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mpwapwa Sarah Kombakulia  ni Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana na Afisa Kilimo wa Bodi hiyo Frank Mfutakamba

 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana kulia akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpwapwa Paul Mamba Swea wakati wa ziara hiyo
 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana katikaati akiwa na Kaimu Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo kushoto wakitembelea shamba la mfano la Magereza
 Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Bryson Mshana katikati akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo ya kutembeleaa shamba la mfano la magereza wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma kushoto ni Kaimu Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo
 Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Korosho nchini Frank Mfutakamba kushoto akimueleza kitu kwenye mmea wa Korosho Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma Mratibu wa Magereza Joseph Mwita Sabayo
Wakiwa kwenye picha ya pamoja.

NA MWANDISHI WETU, MPWAPWA.

MKUU wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma Jabiri Shekimweri amesema wanalitumia zao la Korosho kujenga uchumi,kuimarisha mapato yao sambamba na vyanzo vyengine vya Halmashauri kutokana na kwamba bado ni zao jipya kwao.

Shekimweri aliyasema hayo  wakati akizungumza na viongozi wa bodi ya Korosho nchini waliofanya ziara ya kutembelea wilaya hiyo ambapo pia waliweza kuwatembelea wakulima ikiwa ni mpango wao kupita kwenye maeneo mapya yanayolima zao hilo kuwahamasisha wakulima ikiwemo shamba la mfano la magereza wilayani Mpwapwa.

Alisema hilo linatokana na kwamba agenda ya zao la Korosho ndio wanalisimamia kwa wigo mpana na walikubaliana kwenye Halmashauri ikiwemo Baraza la madiwani ,Vikao vya Kamati ya Ushauri ya wilaya hiyo (DCC) wakiwemo wadau mbalimbali kwamba wajenge uchumi wa wilaya hiyo kwa kutumia zao la mkakati la Korosho.

Alisema katika agenda ya zao hilo wilayani humo hakuna namna nyengine watapata maendeleo kama hawatalichukua kama zaoi lao la uchumi na kuendelea kuhimiza wananchi kujikita kwenye kilimo hicho kutokana na kuwa na faida lukuki.

“Kwa kweli agenda hizi tatu ni kubwa kujenga uchumi kupitia korosho,kuimarisha mapato ya wilaya yao kupitia Korosho na vyanzo vyengine vya halmashauri kwa sababu ni zao jipya,kupitia korosho mnyororo mrefu wanakwenda kutekeleza falsafa pana ya hapa kazi tu ya Mh Rais wetu Dkt John Magufuli”Alisema DC Jabiri.

Alisema uanzishwaji wa zao hilo unafaida nyingi ikiwemo kutengeneza ajira ya kilimo cha biashara pia zao hilo litavutia viwanda vya ubanguaji korosho na hivyo utajibu Tanzania ya viwanda.

“Kwani ukishakuwa na uzalishaji mkubwa sekta nyengine zitakuja zikiwemo za usafirishaji zitaamka na kuinua uchumi wa wilaya ya Mpwapwa,mkoa na Taifa kwa ujumla “Alisema.

Aliongeza kwamba agenda ya pili ni kuanzisha mashamba darasa ambapo vijana wa Boda boda wana ekari 12 ambazo wanalima korosho lakini pia kuanzisha mashamba darasa ili watu waweze kujifunza ili waweze kulima zao hilo.

Hata hivyo alisema mkakati tatu ni kushawishi namna bora ya upatikanaji wa miche kwani wilayani hapo walikuwa na vikundi saba vya uzalishaji ya miche kwa vitalu mwaka jana walizalisha miche 480,000 huku miche 100,000 ikisomwa na maji baada ya mvua kubwa kuonyesha.

Kaimu Mkuu wa Gereza la Mpwapwa Mratibu Magereza Joseph Mwita Sabayo aliishukuru bodi ya Korosho kwa kuwatembelea kwenye shamba lao ambalo lilianzishwa mwaka 2009 likiwa limetueliwa na wilaya hiyo kuwa shamba darasa ambalo wananchi walikuwa wanajifunza kupitia shamba hilo.

Alisema hapo mwanzo mikorosho ilikuwa ikionekana kulimwa mikoa ya kanda ya lakani baadae zao hilo liliweza kuenea maeneo mbalimbali huku gereza hilo wakilima ekari elfu hamsini na tisa wamejidhatiti kuhakikisha wanakuwa shamba la mfano

No comments: