Kigali, Rwanda. Yanga imeanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania baada ya kumaliza mechi za Kombe la Shirikisho Afrika, sasa akili yao ni kupambana na Ligi Kuu Bara.
Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema baada ya kuondolewa Kombe la Shirikisho sasa wanarudisha nguvu yote katika ligi.
Mwandila amesema baada ya mechi ya jana watakuwa na wiki mbili za mazoezi ambazo zitatosha kurudisha makali yao waliyoanza nayo ligi.
Naye mshambuliaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib amesema kwa sasa watahakikisha wanatafuta ushindi mechi moja mpaka nyingine mpaka kieleweke.
No comments:
Post a Comment