ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 18, 2018

Elizabeth Michael : Siwezi Kuwa Mtumwa wa Pesa

Msanii kiwango katika tasnia ya Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anasema kamwe hawezi kuwa mtumwa wa pesa kwa kujaribu kufanya kila kazi ya sanaa.

Lulu ambaye amejizolea umaarufu kupitia sanaa ya maigizo, amesema kushiriki kila sanaa kisa tu unatafuta pesa, huo kwake ni utumwa na anaridhika katika uigizaji pekee.

Anasema hawezi kufanya kazi kama Video Queen au nyingine tofauti na uigizaji kwani atajichanganya, hivyo ni vyema akabaki sehemu moja.

“Nadhani kwa kiwango nilichofika ni wakati wa kushika hiki hiki, siwezi kuwa Video Queen na Actress. Siwezi kuwa mtumwa wa pesa kwa kufanya hivyo Some times ni kuweka tu mipaka ya kazi zako,” alisema.

Anasema kama ni suala la kupata kwa njia ya sanaa, uigizaji unatosha na anafikiria anahitaji kujikita zaidi huko kuliko fani nyingine, kwani anaamini ameandikiwa kupata kupitia huko na si kuhangaika huku na huko akiendekeza pesa na anaamini bila kuwa na msimamo ni rahisi kufanya hata kazi mbaya.

No comments: