ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 6, 2018

HOTUBA YA MHE. KASSIM MAJALIWA (MB) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU MIPANGO NA MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO YASHANGILIWA NA DIASPORA/JUMUIYA YA WATANZANIA SEATTLE, WASHINGTON, MAREKANI.


Mheshimiwa Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico alisoma hotuba kwa niaba ya Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa, MB, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyekuwa amealikwa kufungua Kongamano la Watanzania wanaoishi Marekani, liloandaliwa na DICOTA (Diaspora Council of Tanzanians in America) tarehe 31 Agosti, 2018 hadi tarehe 2 Septemba, 2018 Seattle, Marekani.

Washiriki katika Kongamano la Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani lililoandaliwa na DICOTA (Diaspora Council for Tanzanians in America), wakifuatilia Hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Hoteli ya Seattle Marriott Belleview, Seattle, Washington, Marekani tarehe 31 Agosti 2018 hadi tarehe 2 Septemba 2018.

Washiriki wa Kongamano la Diaspora, Marekani wakishangilia hotuba ya Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa, MB, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoshehini mafanikio na mipango kabambe ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Prof. Dkt. Palamagamba John Kabudi, MB, Waziri wa Katiba na Sheria, akiwasilisha hotuba yake kuhusu tulipotoka baada ya Uhuru, tulipo sasa, tunapoelekea, mafanikio na mipango ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akitoa neno la shukurani baada ya hotuba nzuri sana ya Mheshimiwa Profesa Dkt. Palamagamba John Kabudi, MB, Waziri wa Katiba na Sheria iliyotangazwa moja kwa moja na Shirika la Habari Tanzania (TBC) na kushuhudiwa nyumbani, Marekani na duniani kote.

Picha ya pamoja ya Ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Kongamano la Diaspora, Seattle, Washington, Marekani na viongozi wa DICOTA wenyeji wa Kongamano hilo.

Mhe. Issa Haji Ussi Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, akifunga Kongamano la Diaspora, Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Marekani lililofanyika Seattle, Washington, Marekani.

No comments: