ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 14, 2018

John Guninita kuzikwa Jumatano Septemba 19

Mwili wa Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita unatarajiwa kuzikwa Jumatano Septemba 19, 2018 kijijini kwao Kibaoni, Ifakara mkoani Morogoro.

Guninita ambaye jina lake linabaki katika orodha ya wanasiasa wenye uwezo wa kutenda kile wanachoamini alifariki dunia jana Septemba 13, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mdogo wa marehemu,  Gerald Guninita amesema mwili wa kaka yake utachukuliwa MNH Jumanne  asubuhi, misa ya mazishi itakayofanyika nyumbani kwake Tabata Kimanga.

Amesema, awali Guninita alikuwa anasumbuliwa na kwiwi, kiungulia na baada ya vipimo alibainika kuwa na uvimbe tumboni.

No comments: