Waheshimiwa Mashakimu Wakzi wa Mikoa na Wilaya kutoka Mikoa mitano ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wakiwa kwenye mahakama ya mfano ili kujipima kuona uelewa wao kuhusu Sheria ya Bunge ya Fidia kwa Wafanyakazi kifungu namba 5 [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] naada ya kushiriki mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na kuratibiwa kwa pamoja na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na kufanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba 5-6, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MAHAKIMU
wakazi wafawidhi wa Mahakama za Mikoa na Wilaya kutoka mikoa mitano ya Dar es
Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara, wamefurahishwa na mafunzo ya
kuwajengea uelewa wa Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi yaliyoandaliwa kwa
ushirikiano baina ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi ni Taasisi ya Hifadhi ya Jamii iliyoanzishwa kwa
Sheria ya Bunge, kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi [Sura ya 263
iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] ambapo jukumu lake kubwa ni kutoa fidia kwa
wafanyakazi walioumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi wanazozifanya.
Kutokana
na jukumu hilo la Mfuko, Chuo cha Uongozi wa Mahama Lushoto ambacho ndicho chenye
dhamana ya kutoa mafunzo kwa watumishi waandamizi wa mahakama, kiliandaa
mafunzo hayo ili kuwawezesha viongozi hao wa mahakama wa ngazi za mikoa na
wilaya kuelewa vema Sheria hiyo ili iwe rahisi kwa wao kutoa maamuzi sahihi
endapo mashauri yahusuyo fidia kwa wafanyakazi na shughhuli za Mfuko yatafika
mbele yao. Amesema Mkuu wa Huduma za Sheria wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) Bw. Abraham Siyovelwa.
Wakizungumza
katika mahojiano baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, alisema
“Nimefurahia
sana kupata mafunzo haya, mimi nina nafasi mbili, kwanza kabisa kama
mfanyakazi, lakini pia kama mdau mkubwa
wa Sheria ya Mfuko huu kama hakimu, nimefaidika sana na elimu hii kwani
nimeelewa vitu vingi ambavyo hapo awali sikuwa nikivijua.”
Alisema,
elimu aliyoipata kama mtumishi wa mahakama, ameelewa haki zake za msingi
kuhusiana na Mfuko huo wa Fidia ameridhika na kufurahia kuwa anafanya kazi
katika mazingira ya uhakika na akiamini pia hata wategemezi wake lolote
likimtokea kutegemea na Mungu amepanga nini, basi wategemezi wake wanaweza
kunufaika licha ya yeye mwenyewe.
“Uelewa
nilioupata baada ya mafunzo haya ni mkubwa sana hususan kwenye makosa ya jinai
yameelezwa bayana, na nimeelewa jinsi nitakavyosimamia sheria hii endapo
nitakutana na kesi yoyote itakayoletwa mbele yangu, kwa sababu ninailewe sheria
hii kwa kina.” Alisema
Alishauri
pia Mfuko uendelee kutoa elimu hususan kwa wafanyakazi, kwani wengi hawajui
manufaa ya huu Mfuko.
Kwa
upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Lindi,
Mhe. James Mutakyahwa Karayemaha amesema, mafunzo aliyoyapata yamemfanya apate
uelewa mpana kuhusu sio tu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na namna gani
anapaswa kuisimamia wakati atakapokutana na mashauri yahusuyo Fidia kwa
wafanyakazi, lakini pia amepata uelewa wa faida anazoweza kupata yeye binafsi
kama mtumishi wa umma.
“Nimejua
kuwa mwajiri kwa mujibu wa Sheria hii, anao wajibu wa kujisajili na kuwasilisha
michango ya kila mwezi kwa Mfuko na asipofanya hivyo anatenda kosa la jinai na
adhabu yake ni kifungo, faini au vyote
viwili.” Alisema
Alisema
pia amejua kuwa kama mfanyakazi hapaswi kushwishiwa kwa namna yoyote ile na
mwajiri wake, kutoa taarifa mbili tofauti za viwango vya mishahara, ambapo
taarifa za malipo ya mtumishi zikionyesha kiwango cha juu cha mshahara na
taarifa zinazopelekwa WCF zikionyesha kiwango cha chini cha mshahara.
“Taarifa
hizi zisizosahihi kama hizi ni janga kwa mfanyakazi kwani endapo atapatwa na tatizo
lolote la kuumia akiwa, kuugua au hata kifo akiwa kazini, inapofika wakati wa
kufidiwa, malipo hayo yatazingatia taarifa za malipo ya mshahara zilizokuwa
zikiwasilishwa kwenye Mfuko.” Alisema.
Naye
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara,
Mhe.Godfrey Mwambapa, alisema kimsingi yeye ameongeza weledi kuhusu sheria
inayoendesha na musimamia shughuli za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
“Mfuko
huu nunatuhusu watu wote tulio kwenye ajira na kwakweli unatusaidia hasa kuwa
salama sehemu ya kazi endapo utapatwa na matatizo sehemu ya kazi Mfuko huu
utakuja na kunifanya niishi kama vile nikiwa kazini na kuniondolea magumu yote
ya kimaisha.” Alsiema.
Alisema,
yeye kama hakimu ameweza kuelewa sheria inayosimamia Mfuko na hata kama shauri
lihusulo masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi litamfikia mbele yake yuko katika
nafasi nzuri ya kusimamia sheria hii kwani ameielewa vilivyo.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, mafunzo hayo ni muendelezo
wa mipango ya Mfuko kutoa elimu kwa wadau wote ambapo tayari Mfuko umetoa elimu
kw amadaktari kote nchini, Waajiri kote nchini, lakini pia elimu kwa
wafanyakazi kwenye maeneo yao ya kazi kupitia ziara za maafisa wa WCF kwenye
taasisi mbalimbali hapa nchini.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mkuu wa Chuom cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, (IJA), Mhe. jaji Dkt.Paul Kihwelo, akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya JIA na WCF. Aliyesimama kushoto ni mratibu wa mafunzo, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo hicho, Mhe. Lameck Samson.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Temeke jijini Dar es Salaam, Mhe. Susan P. Kihawe (kuli) akifurahia jambo wakati akizungumza na mwenzake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Ilala, Mhe. Martha Mpaze.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Morogoro, Mhe. Elizabeth Nyembele, akizungumza.
Waheshimiwa mahakimu wakiwa kwenye majadiliano ya vikundi.
Mhe.S.Mwalusamba (kushoto) na Mhe.Godfrey Mwambapa wakifuatilia kwa makini.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mhe. Gofrey Isaya, akizungumza
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Pwani, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Mhe. Batista Kashushe, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Lameck Samson akifafanua jambo.
Hakimu Mkazi wa Mfawidhi Mahakama ya Kilombero/Ifakara Mkoani Morogoro, Mhe. L.Khamsini akisikiklzia kwa makini wakati Mkuu wa Huduma za Sheria wa WCF, Bw. Abraham Siyovelwa (hayupo pichani) alipokuwa akitoa mada.
Majadiliano ya vikundi
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (wapili kushoto), akimkabidhi cheti cha ushiriki, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka, mwishoni mwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo mahakimu wakazi wa mikoa na wilaya yaliyofikia kilele mkoani Morogoro Septemba 6, 2018. Wengine pichani ni Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa. na kulia ni Mhadhiri Msaidizi, Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Lameck Samson.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba, (kulia) na Mkuu wa Huduma za Sheria, wa Mfuko huo, Bw. Abraham Siyovelwa, wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kuwapongeza mahakimu hao baada ya kumaliza mafunzo.
Majadiliano ya vikundi.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, (kushoto), na Afisa Sheria wa Mfuko huo, Bw. Deo Victor wakijadiliana jambo mwishoni mwa mafunzo hayo.
Afisa Sheria WCF, Bw. Deo Victor (aliyesimama kulia) akisimamia majadiliano ya vikundi kuhusu kile kilichofundihswa.
No comments:
Post a Comment