ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 1, 2018

MAKONTENA YA RC MAKONDA YASHINDIKANA KUUZWA

MNADA wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda umefanyika leo Jumamosi, Septemba 1, 2018 katika Bandari ya Dar, lakini imeshindikana kupatikana mnunuzi, hivyo mnada huo utaendelea Jumamosi ijayo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Scolastika Kevala amesema hawajapata mnunuzi wa kontena hata moja lakini wamefanikiwa kuuza bidhaa 10 tu zilizokuwemo kwenye makontena hayo.

Sehemu kubwa ya bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati na vitu vingine.

“Mpaka sasa tayari tumefanya mnada wa makontena yote 20 lakini hayajapata mteja ingawa tumefanikiwa kuuza bidhaa 10 zilizokuwemo kwenye makontena hayo. Hivyo mnada wa makontena utaendelea tena Jumamosi ijayo,” amesema Kevela.

Itakumbukwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango aliagiza makontena hayo kupigwa mnada licha ya RC Makonda kutoa vitisho kuwa atakayenunua vitu vilivyopo kwenye makontena hayo atapata laana kali.

Aidha, mnada wa Makontena hayo unakuja ikiwa ni baada ya RC Makonda kushindwa kuyalipia kodi kiqasi cha Tsh. Bilioni 1.2

GPL

No comments: