Kitendo cha mfanyabiashara Davis Mosha kutofautiana na maafisa wa uhamiaji hakina uhusiano wowote na maelekezo kutoka juu,wapo wapinzani wa serikali hii ya awamu ya tano,na watumishi wasio na uweledi katika kutimiza kazi zao na kulitumia jina la Mkuu wetu vibaya kwa makusudi au wanataka kujenga chuki juu ya Serikali hii na wafanyabiashara au pengine wanataka kujenga taharuki isiyokuwepo.
Binafsi niliyashuhudia haya kipindi kigumu walichopitia wafanyabiashara wengi akiwemo *DAVIS MOSHA* na maafisa wa TRA.
Niliwahi kushuhudia matamko ya hovyo kutoka kwa maafisa wa TRA wakiwa na wafanyabiashara wakiwatamkia vitu vya hovyo.
Kabla ya Mkuu wa Nchi/Rais kulikemea na TRA kuacha mara moja.
Ukisikiliza upande wa DAVIS MOSHA utasikia akilalamika kuwa mafisa wa Uhamiaji walitumia nguvu kuingia katika eneo lake lenye makazi ya watu na ofisi.
Wakati huo huo mafisa wa uhamiaji wanadai walizuiliwa kufanya kazi zao.
Hapa viongozi wetu wa juu wanahusika je?
Afisa huyu wa uhamiaji aliye record hii video alikuwa na lengo gani? au ndo yale yale niliyoyashuhudia Mwenge na kwa nini afisa huyo aliamua kurusha kipande kimoja?
na kwanini uhamiaji wamemfungulia kesi #DavisMosha pale kituo cha mabatini kijitonyama tarehe 31.07.2018 wakati tukio limetokea 01.08.2018?
Hivi #DavisMosha anawezaje kuprotect wapangaji wake wote wenye uraia tofauti tofauti?.
Uhamiaji jana wamefanya uchunguzi wao kupita kila nyumba wamegundua nini?
Tunataka hii tabia ikome kwa maafisa wasiojielewa.
Serikali hii imejielekeza kwenye kuleta maendeleo kwa watu wote,focus yake ni hiyo.
Wapo watu walioamua kwa makusudi kutumia kila matukio kuichafua serikali yetu na Viongozi wetu wa juu.
Yaani serikali iache kupambana na kuletea wananchi maendeleo zaidi ya Milioni 50
Ikapambane na #DevisMosha why?acheni hizo maafisa wa serikali kuweni na upendo na wafanyabiashara wa Kariba ya DAVIS MOSHA watujengee viwanda.
Ushauri wangu Watumishi na maafisa wa serikali
Msiyatumie majina ya viongozi wetu wa nchi vibaya.
Na wala hamna sababu yakufanya kazi kwa kutengeneza taaruki.
Zungumzeni na wafanyabiashara kwa wema tunataka kodi,tunataka Reli,Stigglers Gorge yaani Umeme wa uhakika tupate viwanda tuajiliwe tuliosoma na tusiosoma.
Wapinzani acheni kutumia matukio haya madogo kuwa ndio njia yenu yakuibuka tena kama mmekwama mmekwama tu hakuna namna.
#Jitafakarini Mlipojikwaa
No comments:
Post a Comment