ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, September 19, 2018

Wataalam wakutana ESRF kuzungumzia ukuaji wa miji Tanzania

 Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),  Bw. Deodatus Sagamiko akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Dk Tausi Kida wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete akitoa neno la ufunguzi wakati wa Mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Mussa Martine akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini akiwasilisha Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab)  na kuongoza majadiliano kuhusu athari za kisera katika tathmini ya kitaifa ya mabadiliko kuelekea miji (National Urbanization Transition Assessment -NUTA) wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Yash Ramkolowan wa DNA Economics kutoka Afrika Kusini akiwasilisha Utafiti wa kuoanisha athari za kiuchumi kwa kuangalia njia mbili zinazotumika Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa viwanda wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Gemma Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI), akiwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wa mipango miji wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
 Mratibu wa Maabara inayoshughulikia mabadiliko kuelekea miji Tanzania (TULab) kutoka ESRF, Reshian W. Kanyatila akielezea masharti ya ushiriki katika shindano la utoaji huduma katika majiji.
 Mtafiti Msaidizi na Mratibu wa Miradi wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Bw. Emmanuel Njavike (katikati) akiwasilisha waliyojadili katika kikundi kazi wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakitoa maoni wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam walioshiriki mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) jana jijini Dar es Salaam.
Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Lorah Basolile Madete (kushoto), Mshehereshaji wa mkutano ambaye pia ni Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dr. Jane Mpapalike (katikati) pamoja na Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha miji kutoka nchini Afrika Kusini wakijadiliana jambo wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Bongo Flava, Beka Flava akitoa burudani ya wimbo maalum wakati wa mkutano wa 5 wa maabara ya ukuaji wa miji Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA kuwa katika mazingira ya sasa ya kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kwa kuwa na viwanda ni lazima taifa litakuwa na mabadiliko katika makazi na kwamba miji mingi itachipuka.
Aidha serikali inapotekeleza mpango wake wa pili wa maendeleo  2016/17-2020/21 katika mpango wa muda mrefu wa maendeleo kwa lengo la kuwezesha mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu uwepo wa miji ni wa lazima.
Aidha mazingira duni ya maisha katika vijiji kunafanya watu kuhamia katika maeneo yenye shughuli mbalimbali na hivyo kukuza miji iliyopo.
Hayo yalisemwa na Dk Lorah Basolile Madete, Mchumi Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha kwenye mkutano wa mkutano wa 5 wa jukwaa la ukuaji wa miji Tanzania (Tanzania Urbanisation Laboratory - TULab) ulioambatana na uwasilishaji wa tafiti tatu zilizofanywa na TUlab kuanzia mwaka jana.
Pia alisema tofauti kubwa ya kipato iliyopo vijijini na mijini inafanya maeneo ya jirani na vijiji kubadilika na kuanza kuchukua muonekano wa miji.
“Ndio kusema ni lazima kujiandaa kwa mabadiliko hayo na kuwa na  mpangilio wa kudhibiti ukuaji wa miji, kinyume chake Tanzania haitaweza kuvuna faida katika uchumi, kijamii na kimazingira kama miji itakua ghafla bila mipango mathubuti” alisema Dk Madete.
Katika mkutano huo ilielezwa kuwa kudhibiti miji ni kitu muhimu ikiwa mataifa yanataka kuwa na maendeleo endelevu ya kiuchumi na ustawi wa jamii.
Miji hiyo inatakiwa kupangwa na kukua kwa mujibu wa makubaliano ya dunia kama  yale ya Paris na maendeleo endelevu yaliyokubaliwa na Umoja wa Mataifa.
Pia makubaliano mengine yanayotakiwa kuzingatiwa ni New Urban Agenda, Ajenda ya maendeleo ya Afrika ya 2063, Mikataba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na ule wa Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kwa kutekeleza makubaliano hayo Tanzania itakuwa inajiweka sawa katika uendelezaji wa miji yake katika hali ambayo inaleta tija na kuongeza ufanisi kwa yale yanayofanyika katika mji.
Katika mpango wa pili wa Maendeleo serikali ya Tanzania imesema wazi kwamba inakuwa na miji iliyopangwa na inayotoa huduma kwa ufanisi kama ya utunzaji wa mazingira, uondoaji wa taka na maji taka, mambo ya usafirishaji na nishati safi ya kuaminika.
Hata hivyo imeelezwa kuwa kazi ya kuendeleza miji haiwezi kufanywa na serikali pekee bali na wadau wengine ambao wanatambua thamani ya upangaji miji.
Katika suala la ushirikiano ndilo linafanya uwepo wa Jukwaa la Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) kuwa la muhimu ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya miji kwa kuisaidia Serikali kufanya maamuzi yenye uhakika na tija.
TULab ilianzishwa Agosti 2017 na Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na  ESRF na Coalition for Urban Transitions (CUT) na kufanya tafiti tatu zilizowasilishwa na Bw. Anton Cartwright wa Kituo cha Afrika cha Miji, Afrika Kusini.
Bw. Anton aliwasilisha  Muhtasari wa tafiti tatu zilizofanyika chini ya Jukwaa hilo linaloshughulikia mabadiliko kuelekea miji bora Tanzania au kwa ufupi TULab  na jinsi tafiti hizo zitakavyosaidia kuandaa mwongozo wa ukuaji bora wa miji Tanzania (National Urbanisation Roadmap).
Naye Bw. Yash Ramkolowan  kutoka  Afrika Kusini aliwasilisha Utafiti utakao angalia uhusiano kati ya viwanda na ukuaji wa miji Tanzania huku Gemma Todd kutoka Ifakara Health Institute (IHI) aliwasilisha matokeo ya awali ya utafiti wa mipango miji.
Naye Mratibu wa TULab. Reshian W. Kanyatila, alizungumzia Shindano la Utoaji Huduma Bunifu zitakazosaidia kuboresha Jiji la Dar es salaam na masharti ya jinsi ya kushiriki katika shindano hilo.
Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Mkurugenzi wa ESRF Bw. Deodatus Sagamiko alisema kwamba tangu mwaka jana kuanzishwa kwa TUlab, tafiti tatu zimefanyika ambazo zinafungua ukurasa wa kuanza uandaaji wa mwongozo wa ukuaji bora wa miji Tanzania. Bw. Deodatus Sagamiko, Mkuu wa Utawala na Raslimali Watu wa ESRF, alielezea umuhimu wa tafiti hizo na haja ya kuongeza utafiti mwingine ili kukamilisha maandalizi ya mwongozo huo.
Kutokana na hatua iliyofikiwa TULab inafanya utafiti unaohusisha maendeleo ya viwanda na ukuaji wa miji. Pia TULab inaangalia uwezekano wa kuendesha shindano la ubunifu katika utoaji huduma kwa jiji la Dar es Salaam kabla mwongozo wa ukuaji bora wa miji kuzinduliwa hapo mwakani.

No comments: