ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 1, 2018

TANESCO YATUMIA WIKI YA ZIMAMOTO KUTOA ELIMU DODOMA


 Wiki ya Zimamoti na Uokoaji inataraji kumalizika leo katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma ambapo wadau mbalimbali wakiongozwa na jeshi la Zima Moto na Ukoaji wameshiriki katika maonesho yaliyoenda sambamba na utoaji elimu ya majanga ya moto na uokoaji.

Shirika la Umeme Nchini TANESCo ni miongoni mwa wadau waliounga mkono maaonesgo hayo yakwanza kuanza kufanyika mwaka huu.

Tanesco imetumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusiana na huduma zao wanazotoa lakini kubwa zaidi likiwa ni elimu ya namna ambavyo umeme unaweza kusababisha ajali ya moto na kuteketeza nyumba na majengo.

Mhandisi wa Shirika Hilo anaeshughulika na Afya na Usalama mahali pa kazi, Donart Makingi amesema kuwa yapo mambo ambayo yanaweza kusabnabisha hitilafu katika jengo au nyumba ambavyo ni pamoja na matumizi ya vifaa vya umeme visivyo na ubora, utumiaji mafundi vishoka katika unganishaji umeme, vifaa visivyo na ubora. 

Lakini pia alisema kutumia vitu kama pasi au jiko bila uangalifu na umakini navyo vinaweza kuchangia hitilafu ya umeme na baade nyumba na mali zingine kuteketea. 
Wanafunzi ni miongoni mwa watu waliopatiwa elimu katika Banda la Tanesco.
Maofisa wa Tanesco kutoka idara mbalimbali wapo uwanjani kuhudumia mamia ya wananhi wanao tembelea.
Tanesco inawakumbusha wananchi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mifumo ya umeme walau kila baada ya miaka kadhaa ili kujua kama bado ipo sahihi, 

No comments: