ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 3, 2018

UNAFAHAMU KUWA UNAWEZA KUPATA HUDUMA ZA AIR TANZANIA JUMIA TRAVEL?

Na Jumia Travel Tanzania

Katika jitihada za kurahisisha huduma za usafiri wa anga nchini, Jumia Travel imewasogezea wateja
huduma za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kwenye mtandao wake.
Tunapozungumzia huduma za usafiri wa anga kwa sasa nchini Tanzania hakuna anayeweza kupinga
jitihada kubwa zilizofanywa Air Tanzania. Kuna kazi kubwa imefanywa na shirika katika kuhakikisha
inatoa huduma bora na kubakia kwenye ushindani ndani ya soko. Kwa sasa shirika lina ndege nne
kati ya saba zilizoahidiwa kununuliwa na serikali. Miongoni mwa ndege hizo ni pamoja na Boeing
787-8 Dreamliner ambayo ni ndege kubwa na ya kisasa yenye kubeba abiria wengi zaidi.

Kupitia tovuti ya Jumia Travel wateja wanawezeshwa kufanya huduma za malazi kutoka kwenye
hoteli zaidi ya 1500 katika maeneo tofauti nchini pamoja na kukata tiketi za ndege za mashirika
mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, muda na mahali popote walipo. Njia hii huwarahisishia wasafiri
kuokoa gharama na muda pamoja na kuwaondolea usumbufu wa kwenda moja kwa moja hotelini
au kwenye ofisi husika za mashirika ya ndege.
Kwa mfano, shirika la ndege hivi sasa linatoa huduma zake katika sehemu mbalimbali nchini
na nje kama vile: Dodoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Kigoma, Tabora, Mpanda, Kilimanjaro,
Mtwara, Zanzibar, Pemba, Bukoba na Visiwa vya Comoro.

Siku chache zilizopita Air Tanzania lilitimiza ahadi yake ya kuanza safari za anga nje ya
nchi baada ya ndege zake kutua salama katika viwanja vya Entebe na Bujumbura nchini
Uganda na Burundi ikiwa ni takribani zaidi ya miaka 10 nyuma kufanya hivyo.
Kutokana na kasi ya maendeleo ya teknolojia huduma nyingi zimehamia mtandaoni ili kuwafikia
wateja wengi zaidi na kwa urahisi mahali popote walipo.

Hivyo basi, badala ya msafiri kusafiri mpaka zilipo ofisi za Air Tanzania ili kukata tiketi anaweza
kufanya hivyo akiwa mahali popote na muda wowote alipo. Ni rahisi kwa sababu mfumo
umerahisishwa ili kutumiwa na kila mtu.
Mara tu mteja anapoingia kwenye tovuti ya Jumia Travel itamuhitaji kufuata hatua chache rahisi
ili kukamilisha zoezi zima la kupata tiketi yake ya ndege na kustarehe akisubiria kusafiri.

Kwanza, mteja anatakiwa kujaza taarifa muhimu za awali kama vile: uwanja wa ndege
anaotoka au atakaoanzia safari; uwanja wa ndege atakaotua au kumalizia safari;  idadi ya
abiria pamoja na aina ya safari kama ni kwenda pekee au kwenda na kurudi.

Pili, baada ya kujaza taarifa za awali mteja atabonyeza kitufe kitakachomplekea kupata
machaguo ya huduma mbalimbali za ndege zitakazomfaa. Yatatokea machaguo ya ratiba za
safari za ndege zikiwemo muda wa kusafiri na kufika, pamoja na gharama. Katika hatua
hii mteja ndipo anaamua asafiri na ndege ya muda gani kulingana na mahitaji yake.

Hatua ya mwisho kabisa kwa msafiri anapokuwa mtandaoni ni kujaza taarifa zake binafsi
zitakazokuwepo na kumtambulisha kwenye tiketi yake ya ndege. Tofauti na aina nyingine
ya usafiri, usafiri wa anga huzingatia kwa umakini kabisa taarifa sahihi za msafiri zikiwemo:
majina yake kamili, tarehe ya kuzaliwa, uraia, mawasiliano yake - barua pepe na simu,
aina ya kitambulisho atachokitumia kumtambulisha kama ndani ya nchi basi kitambulisho
cha uraia cha kupiga kura kinatumika wakati kwa safari za nje ya nchi huwa ni pasi ya
kusafiria. Msafiri akishajaza taarifa zote hizi atatakiwa kuchagua njia ya kufanya malipo
ili atumiwe tiketi yake.


Kutokana na hatua mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa na wasafiri wanapotaka kutumia usafiri wa
anga, muda na umakini ni vitu muhimu sana vya kuzingatia. Unatakiwa kuwa makini katika kujaza
taarifa zako binafsi na safari yako la sivyo hautoweza kusafiri. Vilevile, muda nao ni muhimu
kuzingatia hii kwa maana utakapofanya maandalizi ya safari mapema ndivyo utakapopata
bei nafuu pamoja na nafasi ya kujiandaa zaidi na safari.

No comments: