ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 7, 2018

WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA KAZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Kamishna wa Kazi, Bw. Gabriel Malata (wa kwanza kulia). (Kushoto ni) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Andrew Massawe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakimsikiliza Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Andrew Massawe akizungumza jambo walipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama Ofisini kwake Jijini Dodoma, (kulia ni) Kamishna wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Gabriel Malata.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amekutana na Kamishna mpya wa Kazi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu hii leo Septemba 6, 2018 Jijini Dodoma.

Aidha, Waziri Mhagama amemkaribisha Kamishna wa Kazi Bw. Gabriel Malata na kumtaka akasimamie utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa ufasaha.

No comments: