Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipongezwa na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bi. Leah Ulaya (katikati) mara baada ya kumaliza hotuba yake wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Katibu Mkuu wa CWT, Bw. Deus Seif.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoke akizungumza wakati wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). (Wapili kutoka kulia) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa siku mbili kuhusu taarifa ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) leo Jijini Dodoma Septemba 18, 2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akifurahia jambo na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bibi. Leah Ulaya (kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Walimu Wenye Ulemavu (CWT) Taifa, Mwl. Ulumbi Shani (katikati) mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama (Mb) na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bibi. Leah Ulaya (kushoto) wakifurahia jambo na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoka mikoa ya Rukwa na Ruvuma wakati wa zoezi la kupiga picha za pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho leo Jijini Dodoma. Baraza hilo limekutana ili kujadili masuala yanayohusu chama hicho ikiwa ni pamoja na ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG). Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoke.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Taifa la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kutoka mikoa ya Rukwa na Ruvuma mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa dharura wa Baraza la Taifa la chama hicho uliofanyika hii leo Jijini Dodoma.
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (Mb) amewaagiza wajumbe wa baraza la chama cha walimu Tanzania kutekeleza hoja zilizotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Hayo ameyasema hii leo wakati wa kikao cha dhararu kilichowakutanisha wajumbe hao kujadili hoja zote zilizotolewa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) katika taarifa yake ya mwaka 2016/2017.
Waziri Mhagama alieleza kuwa ripoti ya mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) imeelezea changamoto zilizokuwepo kwenye chama hapo awali ikiwemo masuala ya mapato na matumizi ya chama, mfumo wa uongozi na uwajibikaji, mikataba iliyoingiwa na chama ya uwekezaji, suala la utozaji ada kwa wananchana na mfumo wa sera ya malipo ya fedha.
“Wajumbe wa baraza hili mkishiriki kikamilifu katika kujadili na kufikia maamuzi ya pamoja ili kutimiza malengo ya chama na kutakuwa na utaratibu utakao saidia kuongeza uwazi na mshikamano miongoni mwa wanachama” alisisitiza Mhagama.
Aliongeza pia kwa kuyatekeleza hayo chama kitakuwa na utaratibu mzuri utakao heshimiwa na kila kiongozi wa chama na wanachama wote pamoja na namna bora ya kutunza na kutumia fedha za chama ili ziweze kutumika katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa manufaa ya wanachama wote.
Aidha, Mhe. Mhagama alitoa rai kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuangalie mifumo madhubuti ya kutunza kumbukumbu za mali, madeni, michango na idadi ya wanachama kwa kuanzishwa kanzi data “data base” itakayo kuwa inatoa taarifa sahihi.
“Mifumo hii itaondoa malalamiko miongoni mwa wanachama kutokana na upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati, pia utaratibu huu utasaidia kuongeza uwazi na kuleta maendeleo endelevu na kutimiza dhamira ya Chama kwa ujumla” alisema Mhagama.
Kwa Upande wake Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania Bi. Leah Ulaya alisema kuwa hoja zilizotolewa na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali kupitia uchunguzi aliofanya zina manufaa sana kwa chama na hakika zitabadili mwenendo wa chama uliokuwepo awali.
“Tutahakikisha mali zote zinawanufaisha wanachama na tutafuata taratibu kwa kuanzisha mfumo ambao utakuwa thabiti na utasaidia moja kwa moja kumuonesha mwanachama ameshiriki kwa namna gani ikiwemo uchangiaji wa michango yake.” Alisema Ulaya.
Naye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania Bw. Deus Seif alikubali wito wa Waziri kwa kueleza kuwa watajadili hoja zote zilizotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa kina na kuhakikisha wajumbe wote wa baraza watashiriki katika mjadala huo na kufikia maamuzi ya pamoja kwa mustakabali wa chama.
No comments:
Post a Comment