Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.
Na Mathias Canal, NFRA
Zoezi la kununua nafaka ya mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi yasiyokuwa na ubora.
Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka Jana kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa shambani.
Katika hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika kituo hicho.
Katika ziara hiyo ya Mtendaji Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya kwanza ya ununuzi na hadi kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo imeshanunua zaidi ya tani 6000.
Ili kuimarisha dhana ya Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi kupitia vyama ya Ushirika na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS ambazo jumla yake zinakuwa 23 ambazo ndizo zilizobainishwa na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.
Vikundi hivyo vya wakulima ni kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Songea vijijini, Mbinga mji, Mbinga vijijini, Namtumbo na Wilaya ya Nyasa.
Vumilia aonyesha kuridhishwa na hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea kusisitiza na kununua mahindi yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya Hifadhi ya Taifa ya Chakula.
Katika hatua nyingine Bi Vumilia amewapongeza watumishi wa NFRA kwa kazi nzuri ya kiuweledi wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao na wakala kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment