ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 22, 2018

CHUO CHA MISITU OLMOTONYI WAMFIKISHIA KILIO NAIBU WAZIRI MHE.KANYASU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Watumishi  wakati  alipowatembelea leo katika  Chuo cha Misitu cha Olmotonyi jijini Arusha ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aliposhika nyadhifa hiyo.( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Makamu Mkuu wa Chuo cha Misitu cha Olmotonnyi Bw.Steve Kigwere akisoma taarifa  mbele ya Naibu Waziri, Mhe. Kanyasu  wakati alipotembelea leo Chuo hicho kilichopo  jijini Arusha  kwa ajili ya  kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Mkufunzi wa Chuo cha Misitu Olmotony,Charles Giliba akizungumza mbele ya Naibu Waziri Mhe, Kanyasu,   wakati alipotembelea jana  Chuo hicho kilichopo jijini Arusha  kwa ajili ya  kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

Watumishi wa Chuo cha Misitu cha Olomotonyi wamemuomba Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ashughulikie changamoto mbalimbali zinazowakabili   ikiwemo kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupandishwa vyeo. Pia,  watumishi hao wamesema  wamekuwa hawapandishwi vyeo kwa muda mrefu  jambo ambalo limekuwa likishusha ari ya kufanya kazi kwa bidii.

Wameyasema hayo   leo mbele ya Naibu Waziri Mhe. Kanyasu wakati alipokuwa akisikiliza changamoto  za watumishi wa Chuo hicho  jijini Arusha  ikiwa ni mara yake ya kwanza  kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa  kushika wadhifa huo   Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wenzake, Mkufunzi wa Chuo hicho, Philipina Shao amesema  kwa muda wa miaka 12 hajapandishwa cheo  na kwa sasa anakaribia kustaafu.

Mbali na malalamiko hayo,  Watumishi hao wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa Chuo hicho kimekuwa kama gereza kwa vile baadhi ya watumishi ambao wameonekana kufanya vibaya maeneo mengine  huhamishiwa katika Chuo hicho kama adhabu. Wakizungumzia kuhusu  watumishi hao ambao wamekuwa wakihamishiwa  katika Chuo hicho kuwa wengi wao huwa wamebakiza miaka michache kustaafu, hivyo wanakuwa hawana mchango wowote kwa Chuo.

Aidha, Mkufunzi wa Cho hicho,Dkt.Lupala Zacharia  amesema kumekuwa na  ushirikishwaji hafifu kati ya Chuo na Idara ya Misitu na Nyuki hali inayopelekea kujiona kuwa wao sio sehemu ya  Wizara ya Maliasili na Utalii. Ameongeza kuwa kumekuwa na  mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanywa  na Idara pasipo kushirikishwa

Naye Mkufunzi Charles Giliba amesema Chuo hicho kimetengwa kwa muda mrefu hata pale inapotea vikosi kazi vinapoundwa Wizarani vya kufanya kazi fulani wamekuwa hawapati nafasi ya kushirikishwa. "Hatutaki tubebwe, tuna sifa stahiki na tunajisikia tunadhulumiwa haki yetu kwa vile  hatutumiwi ipasavyo" amesema Giliba

Katika hatua nyingine, Wamemueleza Naibu Waziri huyo kuwa hata teuzi zinapotokea  za kushika nafasi za juu katika masuala ya misitu, Chuo hicho kimekuwa hakipati nafasi ilhali kina wataalamu wabobezi na wenye uwezo hali ya juu. Aidha, Watumishi hao wamesema licha ya kuwa Chuo hicho kipo kwenye mfumo wa NACTE lakini hata hivyo Wakufunzi wamekuwa wakilipwa mshahara  kama mafisa misitu kufuatia kukosekana kwa muundo wa utumishi.

Hivyo wamemuomba Naibu Wazi huyo ashughulikie muundo huo ili waanze  kulipwa  stahili zao  kama vyuo vingine ambavyo vipo  katika mfumo huo  Kwa upande wake,Naibu Waziri Mhe.Kanyasu wakati alipokuwa akijibu  kero hizo amewahakikishia Watumishi hao kuwa atazishughulikia baadhi ya changamoto hizo haraka iwezekanavyo.

Pia, Amesema Chuo hicho hakijatengwa ila kumekuwa na mazoea ya viongozi walio wengi kuteua majina ya watalaamu kutoka vyuo vikubwa wakiamini huko ndiko kuna wataalamu. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo ameishauri Menejimenti ya Chuo hicho isikae kimya badala yake isikume  mambo hasa  pale  inapodhani yakifanyika yataweza kuisaidia Wizara pamoja na taifa kwa ujumla.

No comments: