Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi akisalimiana na Balozi wa Namibia nchini, Mhe. Theresa Samaria alipofika Wizarani kwa ajili ya kumsalimia na kuzungumzia kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia kwenye sekta mbalimbali ikiwemo biashara, kilimo, uvuvi na mifugo. Mazungumzo hayo yamefanyika tarehe 19 Novemba, 2018.
Mhe. Balozi Samaria akimweleza Dkt. Kasidi kuhusu fursa mbalimbali za biashara ambazo Tanzania inaweza kuzichangamkia kwenye nchi yake ambayo ina ukame uliokithiri kutokana na kuzungukwa na Majangwa ya Kalahari na Namib. Fursa hizo ni pamoja na biashara ya nyama, matunda, nafaka mbalimbali na korosho.
Katibu Mkuu, Dkt. Kasidi akisoma nyaraka aliyopatiwa na Balozi Samaria ambayo ni mkataba ulioanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Namibia miaka 20 iliyopita.
Dkt. Kasidi akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Samaria mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Piacha ya pamoja kati ya Dkt. Kasidi na Balozi Samaria pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Ubalozi wa Namibia nchini walioshiriki mazungumzo kati ya viongozi hao
No comments:
Post a Comment