Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akifungua mkutano kati ya ujumbe kutoka Makampuni 7 makubwa ya Uturuki na wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji jijini Dar es Salaam ambao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Katika mkutano huo ambao ulifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) tarehe 19 Novemba 2018, Prof. Kiondo alieleza kuwa wawekezaji hao kutoka Uturuki wana nia ya dhati ya kuwekeza hapa nchini kwa kuanzia na mikoa ya Dodoma na Simiyu katika sekta za viwanda vya nguo, uongezaji thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa ya biashara na ujenzi wa hoteli za kimataifa.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Ali Davutoglu nae alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wawekezaji hao mazingira rafiki ya uwekezaji yaliyopo hapa nchini kutokana na uzoefu wake wa kuwepo nchini.
Sehemu nyingine ya wawekezaji hao kutoka Uturuki
Mkutano ukiendelea
Sehemu ya wadau kutoka sekta muhimu za Tanzania nao wakifuatilia mkutano huo
Afisa kutoka TIC, Bi. Diana Ladislaus akiwasilisha mada kuhusu Uwekezaji nchini Tanzania kwa wawekezaji hao kutoka Uturuki
Wadau wakifuatilia kwa makini mada ya uwekezaji iliyokuwa ikiwasilishwa
Wadau kutoka sekta mbalimbali za Tanzania ikiwemo EPZA, TCCIA, TANESCO nao wakifuatilia mkutano
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas Nyamanga (katikati) nae akiwa kwenye mkutano huo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa TIC, Bw. John Mnali
Bw. Nyamanga nae akichangia jambo wakati wa mkutano huo ambapo aliwakaribisha wawekezaji hao nchini
Kiongozi wa Msafara wa Wawekezaji hao, Bw. Cengiz Ertas nae akizungumza na kueleza nia yao ya kuja kuwekeza nchini ambapo alisema kwa ujumla wametenga kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 100 kwa ajili ya uwekezaji huo ambao wanatarajia kuuanza mwaka 2019. Pia alieleza kufurahishwa na taarifa kuhusu mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.
Mwakilishi kutoka TPSF akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa wawekezaji hao
Mhe. Prof. Kiondo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano na wawekezaji hao. Kulia ni Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Davutoglu.
Bw. Nyamanga (katikati) na Bw. Mnali (kulia) wakimsikiliza Mhe. Prof. Kiondo (hayupo pichani) akizungumza na waandishi wa habari
Picha ya pamoja
Mhe. Balozi Ali Davutoglu akisalimiana na Bw. Hassani Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje mara baada ya mkutano kati ya wadau muhimu wa uwekezaji wa hapa nchini na ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji kutoka Uturuki
Wakati huohuo wawekezaji hao wakiongozwa na Balozi Ali Davutoglu walihudhuria maadhimisho ya miaka 30 ya TCCIA yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Wadau kutoka Uturuki na Tanzania kwenye maadhimisho ya miaka 30 ya TCCIA
Kina mama ambao walikuwepo kwenye maadhimisho hayo
No comments:
Post a Comment