Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Serikali pamoja na Chama mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya mkoa,wengine pichani kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara Ndugu Simoni Lulu.
Makamu wa Rais amewasili Mererani leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 5 ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Manyara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay na Mbunge wa Babati mjini Mhe. Vrajilal Jituson.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Hannang Mhe. Mary Nagu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Mererani wilayani Simanyiro mkoani Manyara kwa ziara ya siku 5.
Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti, Wabunge pamoja Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi ambapo alipokea taarifa ya mkoa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Mkoa wa Manyara alimueleza kuongezeka kwa mapato katika mkoa huo sambamba kuongezeka kwa makusanyo mara baada ya kujengwa kwa ukuta.
“Miezi 10 kabla ya kujengwa kwa ukuta tulikuwa tunakusanya milioni 402 na miezi 10 baada ya ukuta tunakusanya bilioni 2.1” alisisitiza Mkuu wa Mkoa.
Makamu wa Rais ameushukuru uongozi wa mkoa kwa mapokezi mazuri na kuupongeza kwa hatua mbali mbali za kimaendeleo pamoja na kuboresha huduma za jamii ikiwemo huduma maalum kwa wazee.
No comments:
Post a Comment