Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018. Mkutano huo wa Bunge la Vijana unafanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Kazi na Ajira katika Bunge la Vijana, Mhe. Victoria Ngowi akijibu swali la mbunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kikiendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Mbunge wa Bunge la Vijana kutokea upande wa Upinzani, Mhe. Julius Mtatiro akiuliza swali Bungeni wakati kikao cha Bunge hilo la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Bunge la Vijana, Mhe. Shabir Bigirwa akijibu maswali ya wabunge wakati kikao cha Bunge la Vijana kinachoendelea katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge la Vijana, Mhe. Zephania Sane akiongoza Kikao cha Pili cha Mkutano wa Bunge la Vijana mwaka 2018, mezani wa kwanza mbele ni Katibu wa Bunge hilo,Bi Alphosina Ambrose akiambatana na Makatibu Mezani.Mkutano huo wa Bunge la Vijana unafanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Wabunge wa Bunge la Vijana wakimsikiliza Waziri wa Elimu katika Bunge hilo Mhe. Riziki Bakari wakati akijibu swali la Mbunge katika kikao cha Bunge hilo la Vijana kinachofanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Viongozi mbalimbali wa Upinzani katika Mkutano wa Bunge la Vijana, wa kwanza kushoto ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika bunge hilo, Mhe. Mrisho Juma Ndili, anayefuata ni Waziri Kivuli wa Elimu Mhe. Saidina Hussein na Mhe. Julius Mtatiro.
No comments:
Post a Comment