ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, November 22, 2018

MHE HASUNGA AWATAKA WATAALAMU WIZARA YA KILIMO KUONGEZA UFANISI ILI KUWA NA TIJA KATIKA UZALISHAJI

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya kilimo)
Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akielezea muundo na majukumu ya wizara ya kilimo kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa akizungumza kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) jana tarehe 21 Novemba 2018. KIkao hicho kiliongozwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga ameshangazwa na miradi mingi iliyopo katika wizara ya kilimo huku ikiwa na uchache wa manufaa.

Amesema kuwa wataalamu mbalimbali waliopo katika wizara hiyo wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa weledi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 21 Novemba 2018 wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wakuu wa Bodi za Mazao na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya kilimo sambamba na Wakurugenzi wa Bodi za ushauri, na Wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala Wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) kikiwa na dhumuni la kufahamiana ambapo washiriki wamepata fursa ya kueleza namna ambavyo kilimo kinaweza kuimarika na kuwanufaisha wakulima nchini
“Lazima tuendelee maana rasilimali watu zipo, wasomi wazuri wapo na tafiti zipo hivyo hatuna sababu ya kushindwa kufanikiwa kwenye sekta ya kilimo” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa

“Kuna watu wamepewa rasilimali kubwa kwa ajili ya kuzifanyia kazi lakini ufanisi wao na tija katika utendaji ni mdogo sana jambo hili halikubaliki lazima tubadilike”

Kwa upande wake Naibu waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akichangia katika kikao hicho alisema kuwa tarehe 4 Juni 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alizindua programU ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) huku kukiwa bado kuna mapungufu makubwa kwenye ASDP awamu ya kwanza.

Alisema kuwa katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya ASDP kulitakiwa kujengwa vituo vya kata vya elimu kwa wakulima vya nadharia na vitendo kwani Vilivyojengwa ni vichache huku vikiwa vimebadilishiwa matumizi tofauti na mtazamo uliotakiwa awali.

Pia alisisitiza kusimamiwa ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wizara ya kilimo ili kukabiliana na soko la mazao katika soko la Dunia.

Vilevile Naibu Waziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa alisisitiza kuwa katika kuimarisha kilimo nchini Tume ya Maendeleo ya ushirika inapaswa kusimamiwa kwa weledi mkubwa kwani mafanikio ya mkulima yapo katika muungano wa pamoja ili kuwa na weledi katika kupanga bei ya mazao wanayolima.

Sambamba na hayo Mhe Bashungwa alisisitiza kuwa serikali inajidhatiti katika kuimarisha masoko ya wakulima nchini kwani wakulima wamekuwa wakizalisha mazao mengi lakini changamoto inasalia kukosekana kwa masoko.

MWISHO

No comments: