Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha katika ziara yake ya kutembelea wadau hao, kutambua changamoto zao na kutoa maelekezo ya uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha na uendeshaji wa miradi yao katika ngazi ya jamii.
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Utaratibu mkoa wa Arusha Bw. Moses Mabula akielezea namna Serikali ya mkoa unavyoratibu na kuyasimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ngazi ya Mkoa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Baraka Leonard akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa mkoa wa Arusha kushoto ni Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga na katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Bw. Ismail Suleiman.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Bw. Ismail Suleiman akieleza namna chombo hicho kinavyoshirikiana na Serikali kuunganisha pande hizo mbili katika utekelezaji wa majukumu ya Mashirika Yasiyo ya Kiserkali nchini NGOs katika kikao kilichowakutanisha Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha na Msajili wa NGOs wakati wa Ziara ya Msajili huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo
Mwakilishi wa Shirika la the Girls Foundation of Tanzania Bi. Esther Happy Mariki akiuliza swali kwa Msajili wa NGOs katika kikao kilichowakutanisha Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arisha na Msajili wa NGOs wakati wa Ziara ya Msajili huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga(kushoto) akijadiliana jambo na mmoja wa wadau wa NGOs mkoani Arusha wakati wa Ziara ya Msajili huyo mkoani humo.
Baadhi ya wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani
Arusha wakimsikiliza Msajili wa NGOs Bi. Neema Mwanga (hayupo pichani)
wakati wa ziara ya Msajili huyo mkoani humo kujitambulisha na kutambua
changamoto za mashirika hayo nchini ili kukuza uwazi na uwajibikaji.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga ameyataka Mashirika hayo
kuwajibika kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatekeleza miradi
wanayoiombea fedha kwa kushirikiana na Serikali.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati alipokutana na wadau wa
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kwa lengo la
kujitambulisha, kujadiliana na kujua changamoto zinazoyakabili
Mashirika hayo katika kutekeleza majukumu yake.
Bi. Neema amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatakiwa
kujiendesha kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchini na kuwa wazi,
kuwajibika ila baadhi ya NGOs zimekuwa zikifanya kazi bila kuzingatia
uwazi na uwajibikaji hivyo kupeleka upotevu wa rasilimali zilizoombwa
kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.
Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo na wadau wa NGOs mkoani Arusha ni
kujadiliana na kupata namna bora za kutatua changamoto zinazoikabili
sekta ya NGOs nchini na kusema kuwa ana imani mkutano huo utatoka na
majibu sahihi yatakayowezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani
Arusha kutekeleza majukumu yake katika misingi ya uwazi na
uwajibikaji.
Msajili huyo amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango wa Mshirika
Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa inatoa ajira kwa watanzania na
kusaidiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia
Miradi mbalimbali katika Sekta za Afya, Mazingira na Kilimo na Sekta
nyingine hivyo kuchangia katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo
la taifa.
Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Mashiriki Yasiyo ya Kiserikali Bw.
Baraka Leonard amesema kuwa Serikali imesikia na kufanyia kazi
changamoto mbalimbali za kiutendaji na ipo katika hatua za mwisho
kuhamishia shughuli za usajili na uratibu wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali nchini katika mfumo wa kidijitali ili kuongeza ufanisi.
“Nisema muda si mrefu tutahamisha taratibu zote za usajili, upokeaji
wa taarifa za NGOs katika mfumo wa kidijitali ili kuendana na kasi ya
mabadiliko ya teknolojia na na kupunguza gharama kwa kurahisisha
utekelezaji wa mambo muhimu kwa kutumia mawasiliano kwa njia ya
kompyuta na simu” alisisitiza Bw. Baraka.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu wa Mkoa wa Arusha Bw.
Moses Mabula Bw. amesema Serikali ya Mkoa inaangalia kwa karibu
uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuhakikisha zinafuata
Sheria ya NGOs, Sheria na taratibu za nchi katika utekelezaji wa
majukumu yao kwa watanzania hasa kwa wananchi wa Arusha kwa
kuhakikisha kile kilichopangwa kinatekelezeka na kuwanufaisha wananchi
hao.
Pia Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO)
Bw. Ismail Suleiman amesema Baraza la NGOs nchini linaendelea kuratibu
masuala mbalimbali ambayo yanawezesha Mashirika hayo kutekeleza
majukumu yao na kuwezesha upatikanaji wa taarifa kati ya NGOs na
Serikali.
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali nchini Bi. Neema Mwanga yupo katika ziara yake
ya kuwatembela wadau wa NGOs nchini ili kujitambulisha na kutambua
changamoto za mashirika hayo katika utekelezaji wa majuku yao ili
kunufaisha wananchi amabo ndio walengwa wakuu.
No comments:
Post a Comment