"Masters" wa Karate toka mitindo tofauti walihudhuria ufungaji wa sherehe ya chama cha Jundokan kilichotimiza miaka 65 na kuwakusanya wanachama wake toka nchi 30 ikiwemo na Tanzania ikiwakirishwa na sensei Fundi Rumadha kwenye Asato Royal Orion Hotel, Naha,Okinawa,Japan.
Katika ufungaji wa sherehe hizo, pia walitunukiwa shahada au Dan wale wote walio pita mitihani yao asubuhi kabla ya sherehe. Ngazi ya juu kabisa katika shere hii kutunukiwa Dan, ni "master" Rony Kluger toka Israel aliyefuzu na kupewa shahada ya dan ya 9 na kuwa na cheo cha "Hanshi".
Meza kuu magwiji wa karate ngazi ya juu kabisa wa Jundokan So Honbu.Masters:
Kancho Yoshihiro Miyazato mwenyekiti wa Jundokan pia ni mtoto wa Eiichi Miyazato, Yasuda sensei, Kinjo sensei, Gima sensei, Higa sensei, Nakada sensei(USA), Renee sensei(France), Merriman sensei(USA) na Gsodam sensei ( Austria).
Master Tetnosuke Yasuda Dan 10, umri wa zaidi miaka 94 na sensei Fundi Rumadha, Asato Royal Orion Hotel
Masters: Meitatsu Yagi wa Meibukan Goju Ryu dan 10, Zempo Shimabukuro wa Shorin Ryu dan 10 na Minoru Higa dan 10 Shorin Ryu pia.
Meitatsu Yagi kulia wa Meibukan Goju Ryu ni mtoto wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chojun Miyagi sensei, Meitoku Yagi mwanzilishi wa Meibukan Goju Ryu, kati ni master wa Okinawa Kobudo
No comments:
Post a Comment