Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Romanus Ishengoma mara baada ya Waziri Kigwangalla kuzindua Bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) wakimkabidhi kabrasha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma (kulia) ikiwa ni ishara ya kumkabidhi majukumu ya kuusimamia Mfuko huo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) wakimkabidhi kabrasha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki wakati Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) wakimkabidhi kabrasha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Tuli Msuya (kulia) wakati Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) wakimkabidhi kabrasha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof, Dos Santos Silayo (kulia) ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wakati Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma. Wengine ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu(wa tatu kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Romanus Ishengoma (wa tatu kulia).
( Picha zote na Lusungu Helela-MNRT)
Na Lusungu Helela-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa mradi wa viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda
Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizindua Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa juu kiutekelezaji.
Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..
Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida kuchochea jamii kuwa mstari wa mbele kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Amesema kiwango cha ufugaji nyuki kwa mikoa inayofuga si cha kuridhisha kwa vile wafugaji walio wengi wamekuwa wakifuga kwa mazoea jambo ambalo wafugaji walio wengi kuamua kuachana na shughuli hiyo na kugeukia uchomaji mkaa pamoja na kujiingiza kwenye shughuli za uharibifu mazingira.
Waziri Kigwangalla amesema uanzishwaji wa viwanda hivyo vitasaidia jamii kuwa na kipato mbadala hali itakayopelekea wananchi kuanza kuona umuhimu wa kulinda na kuhifadhi misitu.
"Mkianza kuwekeza upande wa magharibi ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini wananchi, wakiwemo Nzega, Sikonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua hawatakubali kuona mtu au kikundi cha watu kinaharibu misitu.
"Nataka kuona mapinduzi makubwa kwenye ufugaji nyuki kwa kuiwezesha jamii kuwa na mizinga ya kisasa ili iweze kufuga nyuki kisasa na hatimaye wapeleke kwenye viwanda wakajifunze kufungasha kisasa, ili ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa uhuishaji wa misitu ya kijiji pamoja na ile ya Halmashauri ambayo tayari imeharibiwa kwa kuanza kupanda miti ya asili pamoja na kuanzisha mashamba mapya ya miti.
Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa upandaji miti kwa vile mikoa kama Shinyanga hali ya uharibifu misitu inatisha,
Ameongeza kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa itafika kipidi ambacho akina mama wa vijijjini watakuwa wakitembea umbali wa kilomita 200 kwa ajili yua kutafuta kuni
Awali, Kaimu Katibu ,Mkuu wa Wizara hiyo, Lucius Mwenda amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo umekuwa ukisaidia sana kwenye uhifadhi licha ya kuwa mfuko huo umekuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Romanus Ishengoma amemhakikishia Waziri Kigwangalla kuwa Wajumbe wa Bodi watafanya kazi kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu na kuanza na suala la uanzishwaji wa viwanda vitavyowasaidia wafugaji nyuki nchini.
No comments:
Post a Comment