ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 17, 2018

BARAZA LA KILIMO TANZANIA LAFANYA MKUTANO WAO MKOANI MBEYA

 Mratibu wa Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za TAP II kwa Mwaka 2018 kwa wajumbe waliohudhulia  warsha  ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
 Afisa Masoko wa Ubia wa KIlimo Tanzania Alinanuswe Ambalile aakiwasilisha mada kwa wajumbe waliohudhulia warsha ya wadau wa TAP kuhusu mnyororo wa thamani kwenye mazao.
 Mwakilishi wa Ubia wa kilimo Tanzania kwa  ZONE 1 yenye mikoa ya katavi, songwe na rukwa, Wilson Ernest Loth (wa pili kulia) akiwa na wadau wengine wa TAP wakifuatilia warsha ya wadau wa TAP iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.
Sehemu ya washiriki wa warsha ya siku moja ya wadau wa TAP iliyifanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya.

ZAIDI ya wakulima 1,032 wameanza kutumia Teknolojia ya Kilimo Hifadhi inayomuwezesha mkulima kukabilaina na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kupata mavuno mengi zaidi tofauti na Kilimo cha mazoea cha kutegemea Mvua Pekee.
Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ubia wa kilimo Tanzania mwaka 2018 ulio chini ya baraza la kilimo Tanzania imesema wakulima hao ni kutoka Wilaya za Same, Moshi Vijini, Babati, Monduli na Kiteto ambapo wakulima zaidi ya 2500 walipata mafunzo kuhusu kilimo hifadhi.
Hayo yalielezwa na Mratibu Taifa wa Ubia wa Kilimo Tanzania Mark Magila wakati alipokuwa akizungumza na wajumbe waliohudhulia Warsha ya wadau TAP II iliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilayani Kyela Mkaoni Mbeya ambapo aliwaeleza kuwa teknlojia hiyo inamsaidia mkulima kupata mavuno mengi huku akitumia sehemu ndogo ya ardhi.
“Mpaka sasa TAP II tumekwisha fanikiwa kutoa mafunzo ya stadi za kilimo biashara kwa wakulima 700 kutoka kwa wilaya 7 za Meru, Kiteto, Babati, Kilombero, Morogoro Vijijini, Namtumbo na Songea Vijijini lengo ikiwa ni kuendelea kuwajengea uwezo wakulima nchini,
“Lakini pia AMCO 20  zilijengewa uwezo juu ya masuala ya mikopo na kuwaunganisha na watoa huduma za kifedha kwenye wilaya 10 ambazo ni Sumbawanga, Mpanda, Kyela, Mvomero, Morogoro Vijijini,Kilombero, Ulanga, Mufindi, Iringa na Mbeya” ilisema taarifa hiyo iliyosomwa na Mark Magila mratibu wa taifa wa TAP II.
Wakulima wapatao 800 na wasindikaji 100 walijengewa uwezo huku kwakulima vijana zaidi ya 400 pia nao wakipatiwa mafunzo ya masuala ya kijinsia kutoka katika wilaya 20.
Taarifa hiyo pia ilieleza kwa mwaka ujao TAP II  itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya umma katika kutekeleza ubia wa kilimo ikiwa ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za kilimo.
Wakizungumza wakati wa warsha hiyo wadau hao wa Ubia wa Kilimo Tanzania walisema moja ya changamoto kubwa zinazomkabili Mkulima nchini ni kutokuwepo kwa Sera sahihi za bei za mazao kwani wengi wao wanashindwa kulima kutokanana na kutokutabirika kwa bei.
“ Mimi nalima mahindi mwaka jana nimelima mahindi mengi sana lakini bei imetuangusha saana sasa kwa mwaka huu sifikirii kulima pa kubwa kwa sababu bei ya mahindi ya mwaka huu imenishtua sana huenda nikapata hasara kubwa zaidi mwakani” alisema Gabliel Sabila mkulima wa mahindi kutoka Mkoani Katavi.
“ Kimsingi sisi tunaushukuru sana Ubia wa kilimo chini ya Baraza la Kilimo Tanzania, wametusaidia kupata mkopo kwenye scheme yetu ya katurukila, wametushika sana mkono na bila wao tusingepata mkopo, taasisis za fedha nyingi hazimkopeshi mkulima” alisema mmoja wawakulima wa mpunga mkoani morogoro.
Warsha hiyo ya kila mwaka iliwashirikisha wadau wote wa TAP II kutoka wilaya zaidi ya 20 ambapo ndiko mradi huo wa ubia wa kilimo unafanya shughuli zake ambapo pamoja na masuala mengine wameahidi kuendelea kuwa mabalozi wazuri kwa wakulima kuhusua namna bora zaidi ya kumuinua mkulima katika maeneo wanayotoka.

No comments: