Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro akitoa hotuba ya kufungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro. Kulia ni Afisa wa Elimu Afya Mashuleni kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bw. Avit Maro, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco, Dr. Hamisi Malebo (wa pili kulia) pamoja na Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu (kushoto).
Ofisa anayeshughulikia Masuala ya Mtambuka wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Gerald George akitoa salamu kwa niaba ya wizara wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Ofisa Utawala wa Elimu wa TAMISEMI, Jeanimina Mtitu akitoa salamu kwa niaba ya TAMISEMI wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bw. Herman Mathias akizungumza jambo na washiriki wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Mwelekezi wa Afya ya Uzazi kwa Vijana, Bw. Mshana Elineema akiwasilisha mada inayosema ‘Je changamoto ya mimba za utotoni, UKIMWI ni tatizo linaloangaliwa katika sekta ya elimu?’ wakati wa mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Program Meneja wa kitaifa wa elimu ya afya shuleni wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bw. Clement Mung’alo akisherehesha mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro.
Washiriki wa mkutano wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo uliofanyika Hoteli ya Kingsway mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja.
WADAU mbalimbali katika sekta ya elimu wanaokutana mjini Morogoro, wametakiwa kujadiliana kwa kina kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na Ukatili wa Kijinsia kwa kuangalia taratibu zilizopo sasa za kukabiliana na hali hiyo ili kufanya maeneo ya elimu kuwa salama na chanzo cha mabadiliko ya kitabia.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibamayira katika hotuba iliyosomwa na Afisa wa Elimu Afya Mashuleni wa Wizara hiyo, Bw. Avit Maro wakati akifungua mkutano wa wadau wanaojadili kanuni, taratibu sera za taifa kuhusu mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia maeneo ya shule na vyuo.
Mkutano huo ambao umeelezwa kuwa wa kuongeza kasi kwa sekta za elimu kukabiliana na mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya shule na vyuo ni wa kamati ya uratibu ya kitaifa na uthamini wa masuala hayo na unafanyika mkoa wa Morogoro katika hoteli ya Kingsway.
Msingi wa mkutano huo ni kutafuta mkakati wa pamoja wa kuweza kuhuisha sera hizo kulingana na hali ilivyo kwa sasa ili kuweza kukabili changamoto zilizopo.
Amesema kwamba kuwepo kwa mazungumzo hayo kutasaidia kubadilisha sera na taratibu mbalimbali za kitaifa na mataifa katika kukabili mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia.
Alisema nia ni kuweka maeneo ya shule yenye uwezo wa kutoa nasaha zinazosaidia kupambana na changamoto zinazoambatana na matatizo hayo.
Mkutano huo ambao unatarajiwa kuja na jibu la kuwezesha wadau kushirikiana katika kuratibu na kuangalia masuala ya afya shuleni umedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Aidha mkutano utaangalia uwezekano wa wadau kushirikiana na mradi wa Unesco unaoshirikisha Shirika la Sida na WHO kuhusu masuala ya elimu mashuleni.
Akiwasilisha mada katika mkutano huo Program Meneja wa kitaifa wa elimu ya afya shuleni wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Bw. Clement Mung’alo alisema kwamba nyingi ya kanuni na sera zinazotumika ni zile za mwaka 2004 hivyo ipo haja ya kuangalia hali ya sasa ili kupata mwelekeo mpya.
Haja ya kuwa na mwelekeo mpya unatokana na kasi ya changamoto zinazoletwa na mimba za utotoni, UKIMWI na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya vijana.
Kwa sasa katika nchi zinazoendelea watu 70,000 hufariki kila mwaka kutokana na mimba za utotoni.
Aidha alisema kwamba mdondoko wa wanafunzi katika shule za msingi na sekondari ni mkubwa na kwa jinsi hali ilivyo sasa hivi kwa binti kuwa na mimba ni hatari kwake yeye na maisha yake kutokana na jinsi sheria zilivyo na jamii pia.
Alisema kwa sasa kuna sababu nyingi za mimba za utotoni ingawa kubwa ni balehe, utamaduni na umbali wa wasichana kutembea kutafuta elimu.
Aidha alisema kwamba hadi mwaka 2017, watu milioni 1.5 ambapo asilimia 4.5 wana umri wa miaka 15-19.
Mkutano huo unaofanyika katika mji wa Morogoro unajadili na kuangalia uwezekano wa kuboresha sera, kanuni na taratibu za kitaifa kukabili mazingira ya sasa.
Wakati huo huo Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Bw. Tirso Dos Santos amesema Tanzania ina kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba inadhibiti mdondoko wa wanafunzi hasa wa kike kutokana na mimba za utotoni.
Aidha alisema kwamba takwimu zilizopo sasa ambapo mwaka 2017, 2018 wasichana 4,440 wameshindwa kuendelea na masomo kunaonesha haja ya kuangalia kasoro na kujaribu kuziba ili kutoa mwanya wa maendeleo kwa wasichana.
Alisema katika tafiti vijana wengi wamekuwa wakilalamikia kutopata elimu ya uzazi na wakati mwingine hutolewa ikiwa imechelewa na hivyo kujikuta kwenye matatizo.
Aliwataka washiriki wa mkutano huo kuangalia kwa makini taratibu zote na kuona uwezekano wa kushirikiana na majukwaa yaliyopo kama ya ESA kuona namna bora ya kupeleka elimu kukabailiana na changamoto hizo za makuzi.
Mkutano huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika wizara tatu zinazoshughulikia elimu nchini Tanzania za Tamisemi, Elimu na Afya.
No comments:
Post a Comment