Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (hawapo pichani) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathew Kirama (wa pili kutoka kulia) akifafanua majukumu ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (kulia) alipoitembelea idara hiyo kwa lengo la kufahamu majukumu ya idara na kuhimiza uwajibikaji.
JAMES KATUBUKA MWANAMYOTO,
AFISA HABARI MWANDAMIZI,
OFISI YA RAIS-UTUMISHI NA UTAWALA BORA,
19/12/2018.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA TAYARI KUFANYA KAZI MAHALI POPOTE NCHINI ILI KUWAHUDUMIA WANANCHI
Watumishi wa umma wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yoyote nchini ili waweze kuwahudumia wananchi ambao ndio walengwa wakuu wa huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana na watumishi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa lengo la kufahamu majukumu ya Idara hiyo na kuhimiza uwajibikaji.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, kitendo cha watumishi wa umma kuwa tayari kufanya kazi mahali popote na katika mazingira yoyote bila kujali maslahi binafsi kinaashiria uzalendo kwa Taifa na kinatoa haki kwa wananchi katika maeneo yote hususan ya pembezoni kupata huduma bora wanayostahili.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameitaka Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma kutorubuniwa na baadhi ya watumishi na waajiri wanaoomba vibali vya uhamisho kwa maslahi binafsi hivyo kuathiri utoaji huduma kwa umma.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa ameongeza kuwa, Idara hiyo inatakiwa kujiridhisha na hoja zinazowasilishwa kuombea vibali vya uhamisho kama hoja hizo zina tija na manufaa katika maendeleo ya Taifa.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, watanzania wote wana haki sawa ya kupata huduma bora bila kujali mazingira waliyopo hivyo, ni wajibu wa Idara hiyo kuhakikisha kuwa uhamisho wa watumishi hauathiri mahitaji ya huduma kwa wananchi.
Awali, akielezea majukumu ya idara yake, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama amesema, Idara hiyo ina Sehemu ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Sehemu ya Watumishi Waandamizi na Sehemu ya Huduma na Ushauri wa Kisheria ambazo kwa pamoja zinalenga kufanikisha uendeshaji wa utumishi wa umma kwa kuwezesha Taasisi za Serikali kupata watumishi wenye sifa na weledi unaohitajika kulingana na malengo yanayotekelezwa na Taasisi hizo.
Bw. Kirama amefafanua kuwa, idara hiyo ina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu kwa waajiri na watumishi kuhusu sera, sheria, kanuni na nyaraka mbalimbali za masuala ya ajira katika Utumishi wa Umma, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya sheria ikiwa ni pamoja na kusimamia taratibu mbalimbali zinazotawala utumishi wa umma.
Akizungumzia suala la uhamisho, Bw. Kirama amesema, katika kuleta tija na ufanisi kwenye utumishi wa umma, watumishi wa umma wanaruhusiwa kuhama ikiwa wamezingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo likiwemo sharti la kukaa kwenye kituo kimoja cha kazi si chini ya miaka mitatu na uwepo wa nafasi iliyotengewa fedha kwenye kituo husika. Aidha alieza kuwa, Serikali inaweza kumhamisha mtumishi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma katika maeneo yenye upungufu wa watumishi.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameitembelea Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika Idara na Vitengo vya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kuhimiza uwajibikaji.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 19 DESEMBA, 2018
No comments:
Post a Comment