ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 3, 2019

Jafo apongeza Ujenzi Ofisi za Halmashauri ya Kibiti

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa Selemani Jafo(katikati) akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo aliwa na viongozi wa Wilaya ya Kibiti wakati wa ziara yake Wilayani humo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo(katikati) akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti.
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti linaloendelea kujengwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Kibiti kwa Ujenzi mzuri wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya Kibiti mradi unao tarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu. Waziri Jafo alitoa pongezi hizo Leo hii alipokuwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kibiti Mkoani Pwani.  

Ujenzi huo unaojengwa na mkandarasi SUMAJKT chini ya Mshauri Chuo Kikuu cha Ardhi umemridhisha sana Waziri Jafo kutokana na kuzingatiwa kwa viwango vya ubora katika ujenzi huo. Hata hivyo Jafo ameagiza kuongezwa kwa kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kabla ya mwezi Julai, 2019.

Katika ziara hiyo ya kikazi wilayani Kibiti Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea mradi huo pamoja na mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Kivinja "A" ambao unagharimu shilingi milioni 400. Katika kuhitimisha ziara yake wilayani humo waziri Jafo ameutaka uongozi wa wilaya hiyo kutumia fursa waliyonayo ya tofali nzuri zenye ubora zinazo zalishwa na SUMAJKT katika ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo wameshapokea shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo. 

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Seif Ungando ameishukuru sana Serikali ya DKT. John Pombe Joseph Magufuli kwa msaada mkubwa wa miradi ya maendeleo inayo elekezwa wilayani Kibiti

No comments: