Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa Gereza la Kilimo Idete mkoani Morogoro mwishoni mwa juma mara baada ya kuwasili kituoni hapo kujionea hali ya maandalizi ya mashamba ya kilimo cha mpunga ikiwa ni mkakati wa kuelekea kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu kama yalivyo maagizo ya serikali.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa kwanza kushoto) akiongozana na Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro ACP Sylvester Mrema (wa pili kushoto), Mkuu wa Gereza la Kilimo Idete ACP Nsajigwa Mwankenja (wa pili kulia) na maafisa kadhaa katika zoezi la kukagua maandalizi ya shamba la kilimo cha mpunga gerezani hapo, ambalo ni miongoni mwa magereza yaliyoainishwa kuzalisha mpunga na limepewa malengo ya kulima ekari 700 ambazo tayari zimekamilika kulimwa na kwasasa wanaendelea na zoezi la upandaji.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (wa pili kulia) akiongozana na Mkuu wa Gereza la Kilimo Kiberege (wa kwanza kulia), maafisa na askari mbalimbali alipofanya ziara gerezani hapo kujionea maandalizi ya mashamba ya mpunga yaliyoainishwa katika mkakati wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu. Katika mkakati huo Gereza Kiberege limepewa malengo ya kulima ekari 400 ambapo tayari limekamilisha ekari 280 na maandalizi yanaendelea.
Moja ya tractor aina ya Ursus likiendeshwa Cpl Kadili Mohamed wa gereza Kiberege likiwa katika kuandaa mashamba ya mpunga ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kujitosheleza kwa chakula cha wafungwa na mahabusu.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (mbele) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la zahanati katika gereza la Mahange mkoani Morogoro alipofanya ziara rasmi ya kikazi gerezani hapo mwishoni mwa juma ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kuhakikisha anatembelea magereza mbalimbali nchini kujionea hali halisi ya utendaji kazi katika kituo husika na kufanya mabaraza ya maafisa, askari, wafungwa na mahabusu ili kusikiliza shida zao na kupokea ushauri na mapendekezo mbalimbali juu ya namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike akisalimiana na maafisa wa Gereza la Wilaya Kilosa mkoani Morogoro mara alipowasili kituoni hapo akiwa katika ziara ya kikazi mapema juma hili. Mbali na kutembelea magereza yenye mashamba ya kimkakati Jenerali Kasike ametumia nafasi hiyo kutembelea magereza mengine mkoani humo kujionea shughuli mbalimbali za utendaji kazi ambapo amefanya mabaraza ya maafisa, askari, wafungwa na mahabusu ili kusikiliza kero mbalimbali na kuona namna bora ya kukabiliana nazo.
Baadhi ya askari wa Gereza Mahenge wakifuatilia hotuba ya Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kakazi kituoni hapo. Kamishna Kasike pamoja na mambo mengine aliwataka maafisa na askari kufanya kazi kwa ubunifu, ushirikiano, uhusiano mwema ndani na nje ya jeshi lakini yote yakifanyika kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ili kufanikisha majukumu tuliyokabidhiwa na taifa.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Kilimo Idete na wale alioambatana nao katika msafara wake. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo ACP Nsajigwa Mwankenja na Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro ACP Sylvester Mrema. Wa pili kulia ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Udereva KPF, ACP Lazaro Nyanga na wa kwanza kulia ni SP Aniceth Feruzi wa gereza Idete.
Baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Kilimo Kiberege wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo mwishoni mwa juma kujionea utekelezaji wa mkakati wa kujitosheleza kwa chakula katika zao la mpunga. Wa pili ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Udereva KPF ACP Lazaro Nyanga, wa pili kushoto ni wa Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro ACP Sylvester Mrema. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo SSP Hudson Masawe na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Gereza Msaidizi SP George Lwiza.
Baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Wilaya Kilosa wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) baada ya baraza alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo mwanzoni mwa juma hili. Wa pili kulia ni Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro ACP Sylvester Mrema, wa pili kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Ufundi na Udereva KPF,ACP Lazaro Nyanga, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo SSP Elias Mwinuka na wa kwanza kulia ni ASP Atanas Mvula wa gereza hilo.
Kamishna Jenerali wa Magereza Phaustine Kasike (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa kike wa Gereza Mahenge wilayani Ulanga alipofanya ziara ya kikazi gerezani hapo mapema juma hili. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Gereza hilo SP Stockwell Mlyuka na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Gereza Msaidizi ASP Onesphory Mgalla. (Picha zote na Jeshi la Magereza)
No comments:
Post a Comment