Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange akizungumza na Waandishi wa habari juu ya upotoshwaji unaofanywa na vyama vya upinzani juu ya Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) , Habibu Mchange
Humphrey Shao, Globu ya Jamii
ASASI ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) imesema kuwa muswada mpya wa sheria wa vyama vya siasa uliyotolewa hivi karibuni una lengo la kudhibiti kikamilifu fedha za ruzuku za vyama vya siasa.
Asasi hiyo pia imesema muswada huo kama utapitishwa na kuwa sheria rasmi, utadhibiti ukomo wa uongozi wa juu katika vyama vya siasa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Habibu Mchange alisema kwa sasa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikilaumiwa juu ya matumizi mabaya ya fedha hivyo anaamini uwepo wa muswada huo ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria itadhibiti jambo hilo.
Alisema licha ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuulalamikia muswada huo, yeye kama mwanademokrasia nchini anaamini kuwa sheria hiyo itasaidia kukuza na kuvijenga vyama vya siasa.
“Mimi na asasi yangu pamoja na vijana wenzangu tunamshukuru aliyependekeza muswada huu, kwani huko nyuma niliwahi kukandamizwa nikiwa katika vyama kutokana na kutokuwepo kwa sheria hii.
“Kupitia muswada huu ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria utakwenda kusimamia vema ruzuku za kila chama cha siasa, kwani Sheria inaeleza kuwa Msajili wa vyama vya siasa atatoa ruzuku kwa vyama na kuelekeza namna ya kuzisimamia , nashangaa kwanini baadhi ya vyama vya upinzania vinapinga jambo hili,” alisema.
Alisema demokrasia ni kugombea nafasi na si watu kushikiria madaraka muda mrefu kwa kuwakandamiza wanasiasa waliopo hivyo kwa kupitia sheria hiyo itawafanya wanasiasa wote kuwa sawa.
“Kutugwa kwa muswada huu kutawasaidia wanasiasa wanaoumia ndani ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kuondoa ukilitimba na Umungu watu,” alisema na kuongeza kuwa
“Viongozi wa chama wengi wamekuwa wakijimikisha vyama kwa kudai wanamichango mikubwa ndani ya vyama, sheria hii itaondoa migogoro na kuwa sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi,” alisema.
Aidha alisema Muswada huo utampa nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi za wananchi ipasavyo pasipo kuingiliwa na chama chochote cha siasa.
“Ndani ya vyama vya siasa kuna watu ambao awandi vyeo kila siku wana cheo kilekile, hii yote ni kutokana na uwepo wa mfumo usiokuwa bora wa chaguzi ndani ya chama,” alisema.
Hata hivyo, Mchange amewataka watanzania kutambua kuwa mabadiriko ya Katiba ni pamoja na mabadiriko ya sheria ndogo ndogo ikiwemo ya vyama vya siasa.
“Sheria itakayotungwa itawapa wanasiasa sehemu moja ya kulalamika na kuwaweka kati wanasiasa wote kwa kuongea lugha mojab,”alisema
Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu muswaada huu unafaida kubwa kwa nchi kwani itasaidia kudhibiti fedha za ruzuku na kukuza vipawa kwa wanachama .
No comments:
Post a Comment