ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 10, 2019

Naibu Waziri Shonza Aridhishwa na Maboresho ya Uwanja wa Nyamagana

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Madulu akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza wakati waziri huyo alipotembelea kujionea  maendeleo ya marekebisho ya Uwanja wa Nyamagana jana jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akishika nyasi bandia za Uwanja wa Nyamagana wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo jana jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akizunguka  Uwanja wa Nyamagana  kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo jana jijini Mwanza.
Sehemu ya Uwanja wa mpira wa miguu wa Nyamagana jijini Mwanza.
 Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Bikhu Kotecha akielezea changamoto zinazoikabili Halmashauri hiyo katika kufanikisha ujenzi wa Uwanja wa Nyamagana (kushoto) wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) alipotembelea kujionea maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo jana jijini Mwanza kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Madulu.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi na wadau wa mpira wa miguu wakati alipotembelea kujionea  maendeleo ya marekebisho ya Uwanja wa Nyamagana jana jijini Mwanza, kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyamagana Alfred Madulu na kushoto ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mhe. Bikhu Kotecha.
 Baadhi ya wadau wa mpira wa miguu jijini Mwanza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza (hayupo pichani) wakati waziri huyo alipotembelea kujionea  maendeleo ya marekebisho ya Uwanja wa Nyamagana jana jijini Mwanza.
Picha na WHUSM – Mwanza

No comments: