ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 8, 2019

PTF YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA SERA YA UCHUMI WA VIWANDA KWA KUWAPATIA MIKOPO KUNDI MAALUMU LA WALEMAVU, AKINA MAMA WAJASIRIAMALI NA VIJANA

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) wakati wa ziara ya kikazi alipowatembelea ofisini kwao jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji, ambapo pia alipata fursa ya kujionea wanufaika wa mikopo inayotolewa na mfuko huo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Mkurugenzi wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) Bi. Haigath Kitala mara baada ya mkurugenzi huyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Mwanjelwa katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ziara ilikuwa na lengo la kufahamu majukumu ya mfuko na kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akisikiliza maelezo ya Bi. Rose Kalulika kuhusu bidhaa zinazozalishwa na kikundi cha akina mama cha UWAZI SHALOOM wakati wa ziara ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akishuhudia bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), kikundi cha UWAZI SHALOOM cha akina mama wasindikaji, Kikundi cha MAKINI FOOD SUPPLIES cha akina mama wasindikaji na kikundi cha MAB cha vijana wakati wa ziara yake ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiwasisitiza watumishi wa PTF kutoa huduma nzuri kwa walengwa wa mikopo inayotolewa na PTF wakati wa ziara ya kikazi katika ofisi za PTF jijini Dar es Salaam, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wanufaika hao wa mikopo inayotolewa na PTF.

JAMES KATUBUKA MWANAMYOTO,
AFISA HABARI,
OFISI YA RAIS-UTUMISHI,
0713 360 813
08/01/2019.

No comments: