Muonekano wa mbele wa jingo la ZURA Zanzibar linalojengwa katika eneo la maisara litakuwa na gorofa saba pacha. litakapomalizika ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo ZURA Maisara Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboub Talib, akishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa ZURA Ndg. Haji Kali Haji, akitowa maelezo ya michoro ya picha ya jengo hilo haiko pichani wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwekaji wa Jiwe la Msingi, ikiwa ni shamrashamara za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, wakati akihutubia katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 Mapinduzi ya Zanzibar.
Wafanyakazi wa Zura wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo jipya la Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib akihutubia wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi wa Jengo la ZURA Maisara Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo la ZURA, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo, akipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZURA Ndg.Haji Kali Haji, kulia na kushoto Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib, akitembelea jengo hilo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na Wajenzi wa jengo la ZURA.katika picha ya pamoja baada ya uwekaji wa jiwe la msingi.(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment