ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 6, 2019

Waziri Mbarawa akagua uwekaji wa mifumo ya Maji na Maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara Ihumwa Jijini Dodoma

Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akikagua miundombimu ya maji katika tanki  ambalo litasambaza  maji katika mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa leo Jijini Dodoma.Tanki hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua lita milioni moja. 
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa  akishiriki  ujenzi wa jengo la Wizara yake unaoendelea katika Mji wa Serikali Ihumwa,Jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo  Bw.Barnabas Ndunguru juu ya ujenzi wa kisima cha maji  kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Wizara hiyo katika eneo la Mji wa Serikali.
 Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akiangalia ramani ya uwekaji  wa mifumo ya Maji  katika chanzo ambapo Serikali inachukua maji  na kupeleka katika Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa Jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Dodoma(DUWASA) Mhandisi David Palangyo.
Picha zote na Daudi Manongi,MAELEZO,DODOMA.06.01.2019

No comments: