ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 24, 2019

ATCL ILIPOZINDUA SAFARI ZAKE ZA ZAMBIA NA ZIMBABWE







 Wageni wakisubiriwa kushuka katika ndege hiyo ya ATCL 
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhandisi Isack Kamwele akisalimiana na Waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira, mara baada ya ndege aina ya air bus A220-300 kutua kwa mara ya kwanza katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Robert Gabriel Mugabe kuashiria uzinduzi rasmi wa kuanza safari katika nchi za Zambia na Zimbabwe.
Kaimu waziri wa uchukuzi wa Zambia Mutolwe Kafwaya akikata keki maalum juzi katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kenneth Kaunda Lusaka Zambia wakati wa uzinduzi rasmi wa safari za ndege za Air Tanzania katika nchi hiyo kuanzia Feb.22,kulia  ni waziri wa Uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Izack Kamwelwe,na kushoto ni balozi wa Zambia nchini Tanzania Benson Chali. 
Waziri wa Mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhurua hafla ya uzinduzi wa safari ya  ya shirika la ndege la Tanzania aina ya Airbus A220-300 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe Harare Zimbambwe juzi kulia ni baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria halfa hiyo akiwemo waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Tanzania mhandisi Isack Kamwele.

************
Shirika la ndege la Tanzania ATCL limezindua  rasmi safari za ndege katika nchi za kusini mwa bara la afrika zikiwemo Zambia na Zimbabwe  ambapo imeelezwa kuwa itachangia  kuchagiza maendeleo ya kiuchumi, baina ya nchi hizo tatu na itafungua milango ya biashara lakini pia kupunguza gharama,muda na usumbufu ambao abiria kutoka katika nchi hizo walikuwa wakiupata kwani walilazimika kuzunguka mpaka nchi jirani ili wafike Zambia au Zimbabwe.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati ndege aina AIRBUS A 220-300 ikiruka  kwa mara ya kwanza kutoka  kiwanja cha ndege cha  kimataifa cha  JKN Dar es salaam kuelekea katika nchi hizo  na kutua  nchini  Zimbabwe na Zambia.
Uzinduzi rasmi wa ndege hiyo umefanyika katika viwanja  viwili tofauti kikiwemo kile cha Robert Gabriel Mugabe Harare- Zimbabwe na baadae uwanja wa Kenneth Kaunda Lusaka- Zambia, huku abiria hao wakipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza katika sekta ya anga ambayo zaidi ya miaka ishirini ilionekana kuyumba.
Baadhi ya abiria Mahenye Muya  mfanyabiashara wa pembejeo za kilimo kutoka Arusha alisema kuwa kuzinduliwa kwa ndege hiyo kumewasaidia kupunguza gharama na mzunguko usiokuwa wa lazima ambao awali ili kufika Lusaka  walilazimika kupitia Ethiopia.  
“Kutoka Tanzania mpaka Harare ni kama saa 1.dakika 50 na Lusaka ni saa 1.dakika 45 muda wa safari umepungua  kwa saa tano,unajua sisi wafanyabiashara muda ni pesa kwa kutumia ATCL nimesave muda na pesa”alisema Muya
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano mhandisi Izak Kamwelwe amesema  shirika hilo limedhamiria kujiimarusha katika sekta hiyo kwa kuongeza idadi ya ndege lakini pia kuhakikisha linafika katika nchi mbalimbali barani Afrika na bara la Asia.
“hivi karibuni tutaanza kwenda India ambayo ni mwisho wa mwezi Machi,na mwezi April mwishoni au Mei tutaanza kusafiri kwenda China kwa sababu tupo katika hatua nzuri ya mazungumzo.”alisema Kamwelwe.
Alisema serikali itaendeleza na wimbi la kununua ndege ambapo mwezi November itapokea ndege nyingine aina ya Dreamliner na Bombadier hivyo kufanya serikali ya Jamhuri ya muungano kuwa na ndege 11.
Akizungumzia namna shirika hilo lilivyojipanga katika kutoa huduma hiyo ya anga karika nchi mbalimbali barani Afrika Mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege nchini Mhandisi Ladislaus Matindi alisema ATCL imejipanga kutoa huduma safi na ndege zake ni za uhakika.
“ATC imejipanga kulihudumia soko hilo kwa hiyo hatufanyi majaribio wala hatufanyi kitu tusichokuwa na uhakika nacho tunahakika na hili soko”alisema Matindi
Kwa upande wake waziri wa mazingira na utalii wa Zimbabwe Prisca Mupfumira na kaimu waziri wa uchukuzi na mawasiliano wa Zambia Kafwaya Mutotwe wamesema kuanza kwa safari hizo kutaendeleza  kuimarisha uhusiano uliopo wa muda mrefu uliowekwa na waasisi wa mataifa hayo  katika Nyanja mbalimbali.
“Leo historia inaandikwa tena baada ya miaka ishirini ndege za Tanzania kugusa ardhi ya Zimbabwe naamini uzinduzi huu unatarajiwa kufungua furs azote kuanzia kiuchumi,na raia wetu kufurahia mawasiliano ya uhakika kufikia vivutio vya utalii na biashara”alisema Mupfumira
Ndege hiyo aina ya AIRBUS A 220-300 ya Shirika la ndege la Tanzania itakuwa ikisafiri  mara tatu kwa wiki kuelekea katika nchi za Zambia na Zimbabwe ambapo mpaka sasa ndege hizo zitakuwa zikifika katika nchi nne za Afrika ikiwemo Uganda na Burundi.

No comments: