Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, alipowatembelea wanufaika hao wilayani humo kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo na kupata shuhuda za walengwa.
Baadhi ya wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipowatembelea wanufaika hao kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo na kupata shuhuda za walengwa.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said wakifurahia jambo na mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani (kushoto) nyumbani kwa mmnufaika huyo mara baada ya kumtembelea na kushuhudia cherehani aliyoinunua pamoja na nyumba aliyoijenga kutokana na fedha za ruzuku anazozipata.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said wakiwa nyumbani kwa mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilaya ya Pangani, mara baada ya kuitembelea familia ya mnufaika huyo ili kushuhudia namna fedha za ruzuku zilivyomnufaisha mlengwa huyo.
JAMES KATUBUKA MWANAMYOTO,
AFISA HABARI,
OFISI YA RAIS-UTUMISHI,
0713 360 813
16/02/2019.
Wanufaika wa fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wametakiwa kuzitumia vizuri fedha za ruzuka wanazozipata katika shughuli mbalimbali zitakazowawezesha kujiinua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipowatembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo, ambapo amepata fursa ya kushuhudia kazi za maendeleo za wanufaika wa mpango katika Halmashauri hiyo.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewaasa wanufaika hao kutumia fedha hizo kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za kiuchumi badala ya kuzitumia katika mambo mengine yasiyo ya maendeleo.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewahakikishia wakazi wa Pangani kuwa, katika utekelezaji wa Mpango kwa awamu mpya utakaoanza mwezi Julai, 2019 Serikali itahakikisha kaya zote maskini wilayani Pangani zinanufaika kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameelekeza.
Kwa upande wake, mmoja wa wanufaika wilayani humo, Mama Bwele amesema fedha hizo zimemuwezesha kujenga nyumba ya vyumba viwili na kununua mbuzi wa kufuga wanaomsaidia kuongeza kipato, hivyo amewataka wanufaika wenzie kutumia fedha hizo kwa malengo ili kujikwamua na umaskini.
Naye mnufaika mwingine, Bi. Mariam Mohamed amesema fedha anazozipata zimemuwezesha kusomesha watoto alioachiwa na marehemu dada yake kwa kununua mahitaji ya shule ya watoto hao ikiwemo madaftali na sare za shule.
Bi. Mohamed ameongeza kuwa, ruzuku hiyo pia imemuwezesha kununua bati za kujengea nyumba yake ya vyumba viwili, hivyo ameishukuru Serikali kwa kuzikumbuka kaya maskini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Nchini.
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ameridhishwa na kiwango cha utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani baada ya kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa na wanufaika wa Halmashauri hiyo.
IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 16 FEBRUARI, 2019
No comments:
Post a Comment