Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi kabla ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani kuwasha umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika kijiji cha Ibanda katika wilaya Geita mkoani Geita.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa kwanza kulia) akimueleza Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani ( wa kwanza kushoto) kuhusiana na nguzo ambazo zimerundikwa katika kijiji cha Ibanda ambazo zimekaa zaidi ya mwaka mmoja bila kutumiwa ilhali kuna maeneo mengine ya wilaya hiyo baadhi ya wananchi wamekosa kuunganishiwa umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA kutokana na kukosekana kwa nguzo hizo.Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Geita, Josephat Maganga.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akikabidhiwa kifaa maalum ambacho kinamsaidia mwananchi anayetaka kuunganishiwa umeme bila kusukiwa vifaa vya umeme katika nyumba yake, anaweza kukitumia kwa ajili kuwasha umeme majumbani pamoja na matumizi mengine ya kila siku katika kijiji cha Ibanda katika wilaya Geita mkoani Geita.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani ( watatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa kwanza kulia) wakicheza na kuimba na wananchi kabla ya zoezi la kuwasha umeme katika kijiji cha ibanda
Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ibanda kabla ya zoezi la kuwasha umeme katika kijiji hicho.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Geita, Mhe. Josephat Maganga kabla,Waziri wa Nishati, Dkt. Medald Kalemani kuwasha umeme katika kijiji cha Ibanda.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini wa REA katika jimbo la Geita mjini kwa vile Geita mjini, mjini ni kata mbili tu ikiwemo Kalangalala na Bombambili na maeneo yote yaliyobaki ni vijiji.
Pia, Mhe.Kanyasu amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa mwaka jana, kijiji kimoja tu katika jimbo hilo ndo kimenufaika na mradi huo.
Akizungumza kabla ya kuzindua umeme wa REA katika kijiji cha Ibanda wilayani Geita, Dkt.Meldard Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita mjini kuchelewa kupata umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni mjini na mjini hakuna vijiji bali kuna mitaa.
"Sisi tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Mhe. Kanyasu ndo kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa ni vijiji" Amesisitiza Waziri Kalemani
Hata hivyo, Waziri Kalemani amemhakikishia Mbunge wa Geita mjini kuwa jumla ya vijiji 42 tayari vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani amewaagiza Wakandarasi na Wataalamu wote kuwa hakuna kuruka nyumba wala kubagua nyumba wahakikishe kila mhitaji anaunganishiwa umeme haraka iwezekanavyo.
Aidha, Waziri Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi wa umeme Tanzania(TANESCO
No comments:
Post a Comment