Advertisements

Wednesday, February 20, 2019

MENEJA MAWASILIANO TFS AFARIKI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI

Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Glory Mziray alifariki dunia jana mchana (Februari 19, 2019), wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upandishaji hadhi wa misitu.

Glory amefikwa na umauti wakati akizungumza na waandishi wa habari. Hali yake ilibadilika ghafla muda mfupi baada ya kumaliza kusoma taarifa ya TFS kuhusu upandishaji hadhi wa misitu lakini alipomaliza alionekana kama kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu.

Alikimbizwa katika kituo cha Afya TMJ kilichopo Chang’ombe kwa ajili ya matibabu na baada ya kumfanyia uchunguzi madaktari wakaeleza kuwa Glory amefariki dunia kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.

Upandishaji hadhi misitu

Taarifa aliyoisoma kuhusu kupandishwa hadhi kwa misitu ilieleza kuwa Serikali imeipandisha hadhi misitu saba ambayo ni Itulu, Rondo, Pinndiro, Kalambo, Mwambesi, Aghondi na Kilinga. Alisema TFS inaendelea na mazungumzo na Serikali za vijiji na zinaridhia kuhifadhi misitu yao ambayo kwa kiwango kikubwa imeharibiwa.

Lengo la jitihada hizo ni kuirudishia misitu hadhi yake ili kufanya uhifadhi kwa faida ya sasa na kizazi kijacho. Pia aligusia suala la ufugaji nyuki na kuhamasisha wafugaji kufuga kibiashara kwani TFS wanaendelea kuwatafutia masoko ndani na nje ya nchi.

No comments: