Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima
akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Bw. Shaibu Ndemanga
mara baaya ya kufanya ziara ya kukagua dampo la Manispaa hiyo ili
kujionea uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira. Katika dampo hilo lililopo
eneo la Machole Manispaa ya Lindi Naibu Waziri Sima ameuagiza uongozi wa
Mkoa kusitisha umwagaji wa maji taka katika eneo hilo.
Sehemu ya taka zikiwa zimerundikwa katika dampo hilo bila kuwekewa mkakati madhubuti wa kuziteketeza.
Naibu Waziri Mussa Sima akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Mkoa wa Lindi mara baada ya kukamilika kwa kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Lindi. Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimeweka mikakati ya kuhifadhi ikolojia ya vyanzo vya maji vinanvyochangia maji katika bonde la Rufiji

Na Lulu Mussa,LINDI .
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Lindi kusitisha mara moja hatua ya kumwaga maji taka katika dampo la Halmashauri hiyo.Agizo hilo limetolewa hii leo Mkoani Lindi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua uzingatiaji na Usimaimizi wa Sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004.

Akiwa
katika Halmashauri hiyo Mhe. Sima amejione uchafuzi mkubwa mazingira
kwa Halmashauri ya Lindi kuchanganya taka ngumu na maji taka katika
dampo moja na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kusitisha mara moja utaratibu
huo na kupiga marufuku wananchi kuingia kiholela katika dampo
hilo.“Utaratibu wa kutofautisha taka uanzie nyumbani na katika sehemu za
kukusanyia taka, taka zikiletwa hapa dampo ziwe zimeshachambuliwa, huu
utaratibu wa watu kuingia hapa dampo kuokota chupa za plastiki usitishwe
mara moja” Alisisitiza Naibu Waziri Sima.
Waziri
Sima amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa taka hatarishi kutupwa dampo
kwakuwa hakuna mkakati madhubuti wa kutenganisha taka hizo toka kwenye
vyanzo vya uzalishaji.Ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake katika Mkoa
wa Lindi Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kuongea na Viongozi
mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wakiwemo madiwani na
viongozi wa Serikali za Mitaa kuweka mikakati madhubuti ya kutunza
Ikolojia ya Vyanzo vya Maji ambavyo ni mto Njenje na Parang’andu ambavyo
hutirisha maji yake katika Mto Luwengu ambao humwaga maji yake kati
katika Mto Rufiji.
“Ndugu
zangu sote tunafahamu umuhimu wa hifadhi ya Mazingira na umuhimu wa
Bonde la Mto Rufiji katika uzalishaji wa Umeme wa Uhakika, sisi watu wa
Mazingira hii kwetu ni fursa, maana uzalishaji wa umeme utasaidia
kuhifadhi mazingira kwa kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Nawasihi
wote tuwe mstari wa mbele katika kuhakikisha sisi tunakuwa mfano wa
kulinda vyanzo vya maji.” Sima alisisitiza.
Aidha,
Naibu Waziri Sima pia amepata fursa ya kutembelea Hospitali ya Mkoa wa
Lindi na kuridhishwa na Mtambo maalumu wa kuteketeza taka ulipo
Hospitalini hapo na kuagiza majengo yayojengwa katika Sekta ya Afya
kuweka miundombinu ya kuvuna maji.Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya
kukagua changamoto za kimazingira pamoja na kuweka mikakati ya
kuzipatia ufumbuzi na pia kuhimizi usimamizi endelevu wa Mazingira
kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyochangia maji katika Bonde la
Rufiji.
No comments:
Post a Comment