Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu akifunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola (COL), Profesa Asha Kanwaramwe akizungumza wakati wahafla ya kufunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na TEW)
Serikali imesema kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa sasa ni kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanakuwa na mazingira salama na rafiki katika mchakato wa kujifunza ili kuwawezesha kupata elimu bora.
Kauli ya Serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu wakati akifunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kundi la watoto wenye mahitaji maalum linasaulika hata unapoangalia miradi ya elimu inayoletwa na wafadhili mara nyingi inaangalia matatizo ya mimba au mila kandamizi lakini wanasahaulika, kundi hili ambalo ni wahanga namba moja wa mila hizo kandamizi ambazo zinawakosesha fursa ya kupata elimu.
“Watoto wenye mahitaji maalum wanasaulika hata wenzetu wafadhili wanapokuja kuanzisha miradi mara nyingi wanapenda kuongelea mambo ya mimba na mila kandamizi lakini wanasahaulika kwamba kundi hili la watoto wenye mahitaji maalum ambao unapoongelea mila kandamizi wao ni wahanga namba moja haijalishi kama wamepata mimba lakini tumewawekea alama kutokana na maumbile yao ” alisemaDkt. Semakafu.
Dkt. Semakafu amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia limeweka kipaumbele kwa kundi hili kwa kuhakikisha miundombinu ya shule ambazo zinachukua watoto wenye mahitaji maalum zinapewa kipaumbele katika kuboreshwa, kununua visaidizi vya watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kusoma na kupata elimu yao katika mazingira yaliyoboreshwa na salama.
Aidha, amesema kwamba mkaka ti mwingine wa serikali ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na shule maalum kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ili kuwezesha kuwalinda watoto bora kama watoto wengineiliwawezekujisaidiakatikamaishayaoyabaadaye.
Naye Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola (COL), Profesa Asha Kanwaramwe ataka washiriki wanaoutekeleza muda huo kutoa chakuutekeleza kwasababu yeyote ile kwani unadabadili maisha ya wasichana wengi nakutaka nchi ishiriki kuimarisha elimu masafa ambayo imekuwa msaada mkubwa kwa wasicha na wanaopata mimba.
Mradiwa Girls Inspire unalenga kuzuia ndoa za utotoni unatekelezwa katika nchi za Tanzania, Msumbiji, Bangladesh, India na Pakistani na kufadhiliwa na serikali za Canada na Australia ambapo kwa Tanzania umatekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Shirika lisilo la Serikali Kiota Women Health and Development, (KIHOWEDE).
No comments:
Post a Comment