Vijana hao waliamua kushiriki katika zoezi hilo mapema leo siku ya Jumapili ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi mpango wa Taifa wa Damu Salama chini ya Wizara ya Afya wa kutoa damu ili kuokoa uhai wa wahitaji wa damu katika hospitali nchini.
Akiongoza zoezi la uchangiaji damu Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo Albert Monyo aliwataka vijana katika jamii kuwa na moyo wa kutoa damu ili kuwasaidia wenye uhitaji maana kwa kufanya hivyo kunasaidia kupunguza uhitaji mkubwa wa damu uliopo kwenye hospitali nyingi hapa nchini.
Naye Afisa muhamasishaji Damu Salama kanda ya Mashariki Mariam Juma alitoa rai kwa waamini wa madhehebu mbalimbali na wanajamii kwa ujumla kujenga tabia ya kuwa wanachangia damu mara kwa mara bila kusubiri dharula.
Alisema uhitaji wa damu bado ni mkubwa na Ofisi ya Damu Salama bado hijawahi kuziba pengo la upatikanaji wa damu ya kutosha kwa asilimia mia moja.
Vijana wakitolewa damu
Baadhi ya Vijana wachangiaji damu wakimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana kanisani hapo akimsikiliza Afisa Mshauri kutoka Damu Salama katika majadiliano kabla ya kutoa damu.
Albert Monyo Mchungaji wa Vijana Kanisani hapo alipowaongoza vijana katika zoezi la uchangiaji damu
Afisa mshauri kutoka damu salama akimshauri mmoja wa wachangiaji damu katika zoezi hilo
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara
Mmoja wa wachangiaji wa damu akioesha kadi yake ya wachangiaji mara kwa mara
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo.
Maafisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama walioendesha zoezi hilo
No comments:
Post a Comment