ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 19, 2019

WANADIASPORA WA SAUDIA WAPIGWA MSASA UHAMIAJI MTANDAO

Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah, Bw. Salim Ali Shatri, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akihutubia, kujibu maswali na kutoa ufafanuzi, mwisho kulia ni Mweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania ya Jeddah, Bw. Abdallah Faris.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakiwa mkutanoni. 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident Jeddah. 
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakipata chakula
Wanajumuiya wakipata chakula

Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia “Tanzania Welfare Society” hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza.

Wanajumuiya walipata fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali yakiwemo uwekezaji na uchumi, ajira nchini Saudi Arabia, masomo nchini Saudi Arabia. Aidha, wanajumuiya walipata maelezo kuhusu matumizi ya mfumo mpya uhamiaji mtandao “e-immigration” ambapo walifahamishwa na kutakiwa kuanza rasmi kuomba pasi mpya za kusafiria za ki-electronic, hati za dharura za kusafiria za ki-electronic. Pia wanajumuiya walitakiwa kuwahamasisha wageni kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii, uwekezaji na biashara, na pia sasa wanaweza kuomba viza za kuingia Tanzania kwa njia ya mtandao “e-visa”. 

Wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania.

No comments: