Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (aliyevaa Kapelo) akiongoza ukaguzi wa ujenzi wa madarasa manane yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na michango ya wadau katika shule ya Msingi Msia, kata ya Milepa Wilayani Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (kushoto) akipewa maelezo juu ya marekebisho yanayoendelea katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Msia na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Kalolo Ntila (kaunda suti nyeusi) wakati wa kuyakagua madarasa hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule akichanganya mchanga na saruji wakati ujenzi wa madarsa ya shule ya sekondari Msia ukiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo akikabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa niaba ya umoja wa waalimu wa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Kipeta kwaajili ya wanafunzi ambao vitabu vyao vilirowa na mvua kutokana na mabweni kuezuliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameliagiza jeshi la polisi Mkoani Humo kuhakikisha wanamsaka na kumkamata mganga wa jadi anayesadikiwa kuwaibua na kuwaadhiri wachawi katika bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga.
Agizo hilo limekuja baada ya kufanya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali katika bonde hilo pamoja na kujionea maendeleo na changamoto za shule ya sekondari Kipeta iliyoezuliwa paa pamoja na shule ya msingi Msia iliyobomoka madarasa manne kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali iliyosababisha madhara hayo mwezi Disemba mwaka 2018.
Ameonya kuwa hataki yaliyotokea mkoa wa Njombe yajirejee katika Mkoa wa Rukwa ikiwa bado watu hawajasahau machungu waliyoyapata kutokana na matukio hayo, na kuongeza kuwa mganga huyo wa kienyeji analindwa na kiongozi wa chama cha kisiasa na hivyo kumtaka mkuu wa kituo cha Kijiji cha Kilyamatundu kuhakikisha anamkamta kiongozi huyo hata kama ni wa Chama cha Mapinduzi.
“OCS na vyombo vyako vile fanya upepelezi wa kina na ukamate yeyote yule ambae ametoka nje ya mkoa huu, nje ya Kilyamatundu anayefanya shughuli hizi, kamata weka ndani fanya mahojiano ya kina, na wengine nimeambiwa hap ani viongozi wa vyama vya kisiasa, usijali huyu ni chama tawala, huyu ni nani, kama ukijua kwa uhakika kamata mhoji mpaka kieleweke, sisi hatutaki kuletewa Lambalamba hapa,” Alisisitiza.
Katika hatua nyingine, Wangabo aliwapongeza waalimu, Uongozi wa vijiji husika pamoja na wananchi kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuhakikisha majengo yaliyobomoka na kuezuliwa katika shule hizo yanarudi katika hali yake ya kawaida na hatimae wanafunzi kuendela na masomo.
Pamoja na michango ya wadau mbalimbali iliyohamasishwa na Wangabo ambayo imesaidia kurudishisa mapaa ya majengo ya utawala, mabweni mawili, nyumba sita za waalimu na vyoo vya wasichana na wavulana kwa shule ya sekondari Kipeta na kujenga madarasa manane kwa shule shule ya Msingi Msia, Wizara ya Elimu pamoja kwa ushirikiano na Wizara ya TAMISEMI imetoa shilingi Milinoni 75.2 kwaajili ya kuongezea ujenzi wa madarasa na vyoo kwa shule hizo.
Naye Diwani wa kata ya Milepa Apolinari Macheta alipongeza juhudi za Mkuu wa Mkoa kwa kuhakikisha shule hizo zinakuwa bora zaidi ya zilivyokuwa na kumuahidi kuwa Shilingi Milioni 48.6 walizopatiwa kwaajili ya ujenzi wa madarasa mawili na vyoo matundu sita kwa shule ya msingi Msia atahakikisha kwa ushirikiano wa wananchi watapata darasa jingine kwa fedha hizo.
No comments:
Post a Comment