ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 24, 2019

SIMBA SC (DIASPORA) YAIADHIBU YANGA SC (DIASPORA) 3-0 NA KUBEBA KOMBE LA OLD SCHOOL REUNION 2019

Tamasha la kila mwaka la Old School Reunion ambalo mwaka huu linafanyika Jijini Houston, Texas jioni ya leo limeshuhudia pambano kali la kukata na shoka la mashabiki wa vilabu mahasimu wakubwa wa soka Tanzania , Simba vs Yanga . Pambano hilo hilo lililoanza majira ya saa kumi na mbili jioni lilijaa ufundi mwingi na kujaza idadi kubwa ya mashabiki kutoka Jijini Houston na pande mbalimbali za Marekani pamoja na nchi za Ulaya. Ikiongozwa na kocha mchezaji Shabaan Mwampambe huku ikiwa na wachezaji mahiri kama Captain Rahim Chomba "Wawa", Elvis Dotto Mnyamuru aka Chama, Ronald Okwi, Abou Mwasa "Kagere" Mudhihir Said Tshabalala na Mark Ritchie Maonyesho timu ya Simba Diaspora iliwatandika Yanga Diaspora bila huruma jumla ya magoli 3-0 . Yanga iliyokuwa chini ya kocha Himidy Mshale "Zahera" akishirikiana na Ebra NY aka Mwandila ilisheheni wachezaji kama mkongwe Deo Ngassa, Abdul Mussa "Fei Toto" , Jabir Liganga , Sam Henry aka Dante na golikipa Shaibu Said Kindoki ilishindwa kabisa kupata mbinu za kuupenya ukuta wa Simba uliokuwa ukiongozwa na Rahim Chomba na golikipa wake Hassan Manula.

Simba SC ilipata magoli yake yote katika kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Ronald Okwi dakika ya 26, Mark Ritchie Mao dakika ya 32 na Abou Mwasa Kagere katika dakika ya 42. Pata picha za tukio hilo hapa chini.
Ronald Okwi wa Simba SC (19) akipachika bao la kwanza huku golikipa wa Yanga Shaibu Said Kindoki akishangaa

Abou Mwasa Kagere wa Simba akitafuta mbinu za kumtoka Kenneth wa Yanga 
Kikosi cha Simba SC (Diaspora) kilichowatandika Yanga SC (Diaspora) 3-0 jioni ya leo Jijini Houston-Texas
Yanga SC (Diaspora)


Nahodha wa Simba Rahim Chomba akikabidhiwa kombe la Ubingwa wa Old School Reunion 2019 na Dr Jenga Ngalawa




Sekeseke

Hatari langoni mwa Simba SC





Wakongwe Elvis Dotto na Rahim Chomba




Mark Richie Maonyesho akiwafungisha tela Yanga SC


































































































































































































































































































































































































































































































































































No comments: