Naibu Katibu Mkuu ADC Queen Alithbet Sendiga akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na Chama hicho kuwapa kipaumbele wanawake mkutano uliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Katibu Mkuu Taifa Chama cha ADC Doyo Hassan Doyo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano Mkuu wa Chama hicho Utakaofanyika Tarehe 14/04/2019 katika Hoteli ya Madinatul Bahar Chukwani Wilaya ya magharibi B Unguja ,hafla iliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika
Mkutano wa Chama cha ADC kuelezea juu ya Mkutano Mkuu wa Chama
hicho14/04/2019.hafla iliofanyika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
Na Rahma Khanis
Katibu Mkuu wa Chama Taifa (ADC) Doyo Hassan Doyo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwadhibiti wanasiasa wasiofuta sheria na maadili ya vyama hivyo ili kuepukana na Migogoro inayoweza kujitokeza.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar. Amesema wanasiasa ni vyema kufuata Sheria na Kanuni zilizowekwa ili kufikia malengo na kujiepusha na migogoro isiyokuwa yalazima kwani kufanya hivyo kutapelekea kuimarisha Chama na kufikia malengo.
Lengo la Mkutano huo ni kuwapa taarifa wananchi na Wazanzibar kuhusiana na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 mwenzi huu katika Ukumbi wa Madinatul Bahari Uliyopo Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Aidha amesema katika Mkutano huo Mkuu wa Chama Taifa watazungumzia mikakati mblimbali ikiwemo Uchaguwa Mkuu na kuchagu Viongozi wa chama hicho ili kuimarisha chama na kutia hamasa kwa Wazanzibar.
Akiongezea kutaja mikakati hiyo kuzinduwa mpango mkakati wa chama ambao unajulikana kama ADC Kaya na ADC Shehiya kwa Zanzibar utakao saidia kupata mafanikio na kukiendeleza chama hicho.
Nae Naibu Katibu Mkuu Taifa wa Chama hicho Queen Althbert Sendiga amewataka akina mama kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi za uongozi kwani chama chao kinatoa fursa kwa kila mwenyeuwezo wa kugombea nafasi hizo.
Aidha amesema ADC inaendelea kutenda fursa na haki kwa akina mama kutokana na kutojitokeza kwa wingi akina mama hao kipindi kilichopita.
No comments:
Post a Comment