ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 18, 2019

KONGAMANO LA KARATE-JUNDOKAN ULAYA TANZANIA KUFANYIKA AUSTRIA

Dr. Friedrich Gsodam sensei "Hanshi 9 Dan", sensei Gabriella Jundokan Karate Austria na sensei Rumadha Fundi
Marehemu sensei N C Bomani aliyeileta Karate Tanzania 1973 na mkufunzi sensei Fundi Rumadha.

Chama cha Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” shina la Jundokan lenye makao yake makuu Asato, mji wa Naha, kisiwa cha Okinawa, Japan, kwa mara nyingine tena, kimetoa mwaliko kwa mwakilishi wa tawi la chama hicho nchini
Tanzania “Shibu-Cho Tanzania”, sensei Fundi Rumadha anaye shikilia ngazi ya
Dan 4 kushiriki kongamano litalofanyika mjini Vienna, Austria julai 18 hadi 21,2019. Tokea uteuzi wake kama mkuu wa chama hicho Tanzania, sensei Fundi ameweza kuwa pandisha ngazi wanafunzi wapatao 12 ngazi za Shodan na Nidan hapa Tanzania.
Kutokana na maelezo ya wenyeji wa kongamano hilo mkuu wa chama cha Jundokan Austria Dr. Friedrich Gsodam sensei mwenye kushikilia ngazi ya “Hanshi”, Dan 9, ambaye alijifunza Karate chini ya mwanzilishi wa chama hicho

master Eiichi Miyazato tangu mwaka 1966, ameweza kukiri na kupendezwa na juhudi za sensei Fundi kuwasaidia wana Jundokan wa Tanzania kufikia ngazi za juu katika Sanaa hii ya Karate.
Viongozi wakuu wa chama hicho cha Jundokan na ujumbe wa Japan utaongozwa na mwenyekiti wake Kancho Yoshihiro Miyazato na ujumbe wa masters au magwiji wa Sanaa hiyo wakiwemo master Tetsu Gima Dan 9, na Sensei Yutaka Oshiro toka Okinawa, Japan. Tanzania, chini ya mkufunzi wake sensei Rumadha na Angola chini ya mkufunzi sensei Filomeno ni wataungana na masensei toka

Afrika ya kusini, Madagascar, Israel, Argentina, Chile, na mataifa ya ulaya kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Poland, Ureno, Corscica, Italy, Urusi, Lithuania, Sweden, Azerbaijan, Scotland, Ireland na Hispania.

Waalikwa watawasili siku ya Alhamisi Julai 18, 2019 katika sehemu maalum ya kijitongoji cha Hollabrunn Vocationa College pembezoni mwa jiji la Vienna, Austria. Kongamano hilo la pekee bala la Ulaya, litafunguliwa kwa semina ya masensei wa matawi yote kwa marekebisho na usahihi wa mbinu tofauti na utumiaji mbinu za kujilinda ikiwemo kata za Sepai, Kururunfa, Sesan na Suparinpei.
Siku ya pili itafuatiwa na mafunzo yatayogawanywa kwa ngazi za mkanda mweupe hadi kahawia, kata za Gekisai dai ichi, Gekisai dai Ni, Saifa, Seiyunchin na Shisochin, na Sanseiru mikanda mieusi Shodan ha Sandan ngazi ya tatu, na hali kadharika nngazi ya nne hadi ya nane, Sanchin na Tensho kata. Nk.

Sensei Fundi anapenda kutoa shukrani zake kwa faraja ya kuwa mmoja ya walimu hao mahili kuhudhuria hayo makongamano muhimu katika ulimwengu wa Karate.
Tayari sensei Fundi amesha pata fursa kubwa za kufanya mafunzi kama hayo na masensei au masters wakuu wa Jundokan Karate huko Leeds, UK, Lisbon, Ureno, Warsaw, Poland na hivi karibuni huko Okinawa, Japan. Pia vilevile, sensei Fundi ataelekea Warsaw, Poland akifuatana na mkewe kwa mwaliko maalum toka mkuu wa Jundokan Poland, sensei Monia Wysocka mwenye Dan 6.
“Lengo na tumaini la Jundokan Tanzania, ni kuwa na walimu wa ngazi za juu wa Karate walio mahili katika sanaa na wanaotambulika chini ya baraza la chama hicho huko Okinawa, Japan”, alisema sensei Fundi.

No comments: