Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza na wananchi wa Arumeru na kumtambukisha RPC mpya mkoa wa Arusha kwa wananchi wa Arumeru ambapo alipata pia nafasi ya kusikiliza kero za wananchi ikiwemo ya Ardhi. Picha na Vero Ignatus.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akizungumza mara baada ya kutambulishwa kwa wananchi wa Arumeru na mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro.
Mkuu wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shanna akizungumza na wananchi wa Arumeru (hawapo pichani) mara baada kusikiliza changamoto zinazohitajika kutatuliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya hiyo.
Na Vero Ignatus, Arumeru.
Mkuu wilaya ya Arumeru Jerry Muro amewahakikishia wananchi wa Arumeru kuwa wataendelea kutatua kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo migogoro ya Ardhi.
Ameyasema hayo wakati akimtambulisha RPC mpya wa mkoa wa Arusha Jonathan Shanna alipotembelea ofisini kwake leo na kuzungumza na wananchi.
Jerry amesema ofisi yake imeweka mkakati wa kuwasaidia wananchi kwa kuwaajiri wanasheria wanne ambao anawalipa kwa kutoa sehemu ya mshara wake kwaajili ya kuwasaidia wananchi wasiokuwa na uwezo wa kupata haki zao.
Wakati huo huo RPCJonathan Shanna amemuagiza mkuu wa polisi wilaya Arumeru SSP Hamisi Mwampelwa, kumsimamisha kazi mara moja mkuu wa kituo cha polisi Kikatiti Inspector Michael Magere kwa kushindwa kusikiliza kero za wananchi wanapo kituoni hapo
Shanna akizungumza na wananchi wa Arumeru amewahakikishia kuwa atawaondoa askari ambao watakiuka taratibu wa jeshi la polisi bila kujali cheo alichonancho.
No comments:
Post a Comment