Majukumu na Madaraka ya Mwenyekiti wa Kitongoji.
Huchaguliwa na wakazi wa kitongoji katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa kitongoji.
Ni mjumbe wa halmashauri ya kijiji kwa wadhifa wake.
Ni kiongozi miongoni mwa viongozi wa kijiji.
Kiungo kati ya halmashauri ya kijiji na wakazi wa kitongoji.
Kuimarisha umoja na mshikamano kati ya serikali ya kijiji na wanakijiji.
Kuwasilisha maoni, mapendekezo na mahitaji ya kitongoji kwa halmashauri ya kijiji.
Kuwasilisha taarifa za halmashauri ya kijiji kwa wakazi wa kitongoji.
Kuitisha mikutano ya wakazi wa kitongoji pale anapoona inafaa.
Mikutano ya kitongoji haina uwezo wa maamuzi inaendeleza mijadala na kuandaa maoni na mapendekezo tu.
Kuhamasisha wakazi wa kitongoji kwenye maendeleo.
Kutunza rejesta ya wakazi wa kitongoji.
No comments:
Post a Comment