ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 9, 2019

TASWIRA MBALIMBALI KWENYE KONGAMANO LA DIASPORA LA TDC GLOBAL, SWEDEN

Wageni mbalimbali kutoka Tanzania wakiongozwa na Mhe. Spika wa Bunge Job Ndugai, Mhe. Salum Maulid (katibu mkuu ofisi ya Rais Zanzibar), Balozi Amisa Mbega(mkurugenzi desk la Diaspora Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano Afrika mashariki) pamoja nao wakiwa na mwenyeji wao Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dr. Wilbroad Slaa wakiwa meza kuu katika kongamano la Diaspora lililoandaliwa na TDC Global siku ya leo Jumanne April 9, 2019. Kongamano hilo linalofanyika ndani ya meli ya abiria linatarajiwa kumalizika siku ya Alhamisi April 11, 2019.
Wadau mbalimbali wakiwemo Diaspora kutoka kila pembe ya Dunia wakishiriki kwa mara ya kwanza katika kongamano hilo la kihistortia.
Wadau wakifuatilia kongamano.
Loveness kutoka DMV katika picha ya pamoja na Hassan Nganzo kutoka Norway.
Kushoto ni Loveness na kulia ni Asha kutoka DMV wakiwa katika picha ya pamoja na Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Askofu mkuu wa Dar es Salaam ambao nao kwa pamoja walikua miongoni mwa wahudhuriaji kwenye kongamano hilo.
Wakati wa chakula.
Menu ikiendelea.

Wageni wakiwasili kwenye meli mapema leo asubuhi.
WanaDiaspora wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai.
Wanamitindo watakao onyesha vivazi kwenye kongamano hilo kutoka kushoto ni Neema kutoka Ufaransa, Asya Idarous Khamsin kutoka Houston, Texas na Mikaela Kutoka Tanzania
Picha zaidi baadae

No comments: