ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 10, 2019

Soko la Ungindoni ni Matokeo chanya ya Juhudi za Serikali ya Mtaa Ungindoni


Mwananchi ana wajibu na majukumu yake kuhakikisha kuwa Kiongozi aliyemchagua au kuteuliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo katika viwango vinavyokubalika katika eneo la kijiji/mtaa kulingana na mipango na makubaliano ya vikao vya kisheria vya kijiji na mtaa. 

Kila mwananchi ana wajibu wa kupinga na kukataa kila aina ya uovu katika jamii ikiwemo rushwa, uonevu, wizi, ubadhirifu wa mali za umma na ya watu binafsi.

Wananchi pia wana jukumu la kudai na kupigania haki zao na za wananchi wengine, kutoa malalamiko na kuuliza maswali juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea kijijini au kwenye mtaa kupitia vyombo mbalimbali vya kijamii na kiserikali. 

Wananchi wanashiriki katika serikali za mitaa kupitia
vikao au mikutano mbalimbali ambapo hujadili na kutoa mapendekezo yao kuhusu mipango na matatizo yanayowakabili kwa namna moja au nyingine ili kuweza kupatiwa ufumbuzi na kurahisisha uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo yao wanamoishi.

Kitabu hiki kimeandaliwa ili kumhamasisha na kumwezesha mwananchi wa kawaida kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazomhusu katika ngazi ya kijiji/mtaa. 

Kitabu hii kinamwonyesha mwananchi wajibu na majukumu
aliyonayo kwa jamii yake anapoishi na pia kinampa haki zake za msingi za kushiriki katika mikutano na vikao mbalimbali vya kisheria katika eneo lake. #MtaaniKwetuPamenoga #MatokeochanyA+ #UchaguziSerikaliZaMitaa2019  

No comments: